Madrassat Swifat Nnabawiyatil Karimah ya Kilimani Zanzibar imefanya
ziara Maalum ya kuwakagua Wagonjwa na kuzuru Makaburi ya Masheikh na la Rias
Alhaj Ali Hassan Mwinyi kwa ajili ya kuwaombea Dua.
Ziara hio iliyoanzia katika Madrassa yao ya [Msolopa] iliopo Kilimani Walianza kwa kumjuilia Hali mmoja kati ya Masheikh wakubwa wa Zanzibar Sheikh Ali Hemed Jabir maarufu maalim Aliyan Mtaa wa Mchangani Mkoa wa Mjini Magharibi ambapo nae akawapa nasaha juu ya kushikamana na Ibada .
Baadae ziara ikaendelea Mangapwani kwa kuzuru Kaburi la Ahajj Ali Hassan Mwinyi aliekua Rais wa Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa awamu ya 3 wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na wakamuombea Dua.
Ziara hio ikamalizia kwa kuzuru Makaburi ya Mlezi na Mwalimu wa Madrassa hio Marehemu Bi.Mwanajuma Jumaane na Marehemu Ustadh Mustafa Iddi Eneo la Mfenesini na Tunguu.
Katika Ziara hio Sheikh Salum Khamis Shafii (Salum Maridhiya] ndie aliewongoza Waalim na Wanafunzi hao katika ziara hio ambayo ni utaratibu waliojiwekea kwa kila mwaka.
Kuwaombea Dua Masheikh mbalimbali na kuzuru Makaburi ni miongoni mwa matukio yaliyowekwa na madrassa hio kwa ajili ya Maadhimisho ya Uzawa wa Mtume Muhammad [Salla lwahu alayhi wassallam ] pamoja na kutimia miaka hamsini ya Madrassa ya Msolopa tangu ilipo asisiwa mwaka 1975.
No comments:
Post a Comment