Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla Kujumuika na Wananchi Katika Maulid ya Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) Viwanja Vya Madungu Chakechake Pemba

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj. Hemed Suleiman Abdulla akitika ubani kuwarehemu Wazee wakati wa hafla ya Maadhimisho ya Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad ( S.A.W ) Mwezi 11 Mfungo Sita (6) 1447 Hijria sawa na Tarehe 04.09.2025 Miladia  yaliyofanyika katika kiwanja cha Polisi Madungu Chake Chake Pemba.

Wazazi na walezi wametakiwa kushirikiana na walimu wa madrasa katika kuwaendeleza vijana wao kwenye mambo ya khairat ikiwemo kusoma maulidi na kumtukuza Mtume Muhammad ( S.A.W)

Hayo yamesemwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla katika maadhimisho ya Maulid ya kuzaliwa kwa mtume Muhammad (S.A.WA ) Mwezi 11 Mfungo sita mwaka 1447 Hijjiria yaliyoyanyika katika Kiwanja cha Polisi Madungu Chake Chake Pemba.

Amesema kuwalea vijana katika malezi bora yenye kufuata mafundisho yaliyomo ndani ya kitabu kitakatifu cha Qur-an pamoja na kuwafundisha mambo mema ikiwemo kusoma maulidi kutapelekea kupata kizazi chema chenye kumcha Mwenyezimungu na kumtukuzaa mtume Muhammad (S.A.W ).

Alhajj Hemed amefahamisha kuwa ni lazima walimu wa madrasa kuhakikisha wanaendeleza kusoma maulid kila ifikapo mfungo sita ili kuendelea kudumisha  mila na silka za kiislamu pamoja na kuwafunua vijana kama walivyofanya wanazuoni waliopita kabla yao.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewataka watu wenye uwezo kuwasaidia walimu wa madrasa katika kufanya maulid kila ifikapo mfungo sita jambo ambalo linapelekea kuzidisha upendo na mshikamano baina yao.

Sambamba na hayo Alhajj Hemed amewasisitiza waumini wa dini ya kiislam na wazanzibar kwa ujumla kuendelea kuitunza  amani na utulivu uliopo nchini unaopelekea kufanya harakati mbali mbali za kidini na kimaendeleo ikiwemo kukusanyika kusoma maulid na kumswalia Mtume Muhammad (S.A.W).

Aidha makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewasisistiza wananchi wa Pemba kutokubali kutumiwa vibaya na wanasiasa kwa maslahi yao binafsi na kutokuitakia mema Zanzibar.

Kwa upande wake katibu mtendaji ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Khalid Ali Mfaume amesema kuwa ofisi ya Mufti wa Zanzibar itaendelea kuratibu na kusimamia shughuli zote za kidini ikiewemo kuadhimisha kuzaliwa kwa mtume Muhammad ( S.A.W ) kwa kusoma maulid kila ifikapo mfungoo sita.

Sheikh Mfaume amewataka waumini wa dini ya kiislamu na walimu wa madrasa kuwa wamoja na kudumisha mapenzi baina yao ili kuendana na sifa alizokuwa nazo mtume Muhammad ( S.A.W ).


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj. Hemed Suleiman Abdulla akizungumza na waumini wa dini ya kiislamu katika Maadhimisho ya Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad  ( S.A.W ) Mwezi 11 Mfungo Sita (6) 1447 Hijria sawa na Tarehe 04.09.2025 Miladia  yaliyofanyika katika kiwanja cha Polisi Madungu Chake Chake Pemba.






Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)

Leo tarehe..05.09.2025.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.