Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambe ni mgombea mteule wa nafasi ya uwakilishi jimbo la kiwani Ndugu Hemed Suleiman Abdulla amewashukuru wanachama wa CCM wa jimbo hilo kwa kuwaunga mkono, kuwaamini na kuwachagua kuwa wagombea katika jimbo hilo.
Ameyasema hayo alipokuwa akisalimiana na wanachama wa CCM wa Tawi la Kendwa mara baada ya kumaliza kuchukua fomu ya kugombe nafasi ya uwakilishi Jimbo la kiwani katika ofisi za Tume ya Uchaguzi Wilaya ya Mkoani.Ndugu Hemed amewataka wanakiwani kuendele kuwa watulivu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi mkuu kwa Kudumisha umoja, amani na mshikamano uliopo kama Katiba ya CCM inavyoelekeza kufanya hivyo kutazidi kukiletea ushindi chama cha Mapinduzi.
Amewakumbusha wananchama wa CCM na wananchi kwa ujumla kuendelea kukumbushana umuhimu wa kuitunza amani iliyopo nchini ikizingatiwa kuwa wazanzibari wote ni ndugu na pia kuna maisha baada ya kumalizika kwa uchaguzi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mkoani ndugu. Ali Juma Nassor amewataka wanachama wa CCM na jumuiya zake pamoja na wapenda Amani na utulivu kuzidisha umoja na mshikamano ambao ndio silaha kubwa ya kukiletea ushindi wa kishindo Chama cha Mapinduzi.
Amesema CCM ipo tayari kuwapokea na kuwakaribisha wanachma wapya kutoka vyama vya upinzani kuja kujiunaga na CCM ili kuendeleza harakati za maendeleo zinazofanywa na viongozi waliopo madarakani.
Nae Mwenyekiti wa CCM Jimbo la Kiwani Ndugu Ali Juma Nassor amewataka wanachama wa CCM wa jimbo hilo kuvunja makundi waliyokuwa nao na kuwaunga mkono wagombea walioteuliwa na chama ili kukitaftia kura nyingi Chama cha Mapinduzi zitakazowawezesha Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na Rais Dkt Hussein Mwinyi kurudi madarakani.
Mwenyekiti Omar amewataka wana CCM Kuacha fitma na majungu na badala yake waungane pamoja katika kukitumikia chama hasa katika wakatika huu wa kuelekea uchaguzi.
Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR )
Tarehe 05.09.2025
No comments:
Post a Comment