Habari za Punde

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mhe. Hemed Suleiman Abdulla Amefungua Kongamano la Mafunzo ya CCM Mkoa wa Kusini Pemba

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu Hemed Suleiman Abdulla akifungua Mafunzo Maalum kwa wagombea wa CCM wa nafasi za Ubunge, Uwakilishi na Udiwani yaliyofanyika katika Ukumbi  Makonyo, Wilaya ya Chake-Chake  Pemba.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu Hemed Suleiman Abdulla amewataka wagombea wateule wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  kuyatumia vizuri mafunzo watakayopatiwa ikiwemo jinsi ya kufanya kampeni na sifa za kiongozi bora ili kuleta tija kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

Ameyasema hayo katika hafla ya ufunguzi wa mafunzo maalum kwa wagombea wa nafasi za Ubunge, Uwakilishi na Udiwani wa Chama cha Mapinduzi katika ukumbi wa Wawi Makonyo wilaya ya chake chake  Pemba.

Amesema kila mteuliwa wa nafasi anayogombea anatakiwa kutambua kuwa tayari amevaa koti la uongozi, hivyo ana wajibu wa kuzifahamu na kuziishi sifa za uongozi na kiongozi bora.

Amesema miongoni mwa sifa za kiongozi bora ni kujiamini, kuwa na matumizi mazuri ya lugha na kuwa na fikra bunifu na  maono juu ya namna ya kutatua changamoto na kuleta maendeleo kwa wananchi.

Amewasisitiza kusimamia vizuri watu na rasilimali, kuwa wastahamilivu hasa kwa kuwa watashirikiana na watu wenye hulka na tabia tofauti na kukutana na changamoto nyingi ambazo zinahitaji uvumilivu katika kuzitatua.

 Aidha, amewataka kuzingatia nidhamu na utayari wa kuleta mabadiliko, usawa, kujiendeleza kielimu   na kuwaunganisha watu na sio kuwagawa kwa maslahi binafsi.

Kwa upande wa kampeni, ndugu Hemed amewasihi wagombea wateule kuzingatia mipaka ya majimbo yao,  kwa kuitambua mitaa, vijiji, shehia na wadi ili wanapozungumza  wasiwe wageni wa kuelezea maeneo yao jambo litakalosaidia kutambua miradi ya maendeleo iliyopo katika jimbo na  wadi pamoja na changamoto zake.

Amewataka kuhakikisha wanatoa ahadi zenye kutekelezeka na si vyenginevyo na   kuhamasisha amani na mshikamano ambao ndio msingi wa mendeleo.

Aidha amewaomba kuitumia vyema fursa hiyo kwa kujifunza, kuuliza maswali, kuchangia na kubadilishana uzoefu ili kila mmoja  abadilike katika mfumo wake wa kimaisha na kiungozi na katika uendeshaji wa kampeni.

Sambamba na hayo amesema anaami kuwa mafunzo hayo yataleta tija ikiwa ni pamoja na kufanyika kwa kampeni za kistaarabu zenye kuinadi Ilani  ya CCM na maendeleo yaliyofanyika na kuhakikisha CCM kinapata ushindi wa kisndo.

Kwa upande wake Katibu wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba ndugu Kajoro Vyohoroka amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo na kuwaongezea maarifa wabunge wateule juu ya namna watakavyoyamudu majukwaa na kuwasilisha hoja zenye kueleweka na kutekelezeka kwa wananchama wa CCM na wananchi kwa ujumla.

Kajoro amesema Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Pemba kimejipanga kuhakikisha majimbo yote tisa (9) ndani ya Mkoa huo yanachukuliwa na CCM pamoja na kuaahidi kura nyingi na ushindi wa kishindo kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt. Samia Suluhu Hassan na Makamu Mwenyekiti wake kwa upande wa Zanzibar Dkt Hussein Ali Mwinyi pamoja na wagombe wa nafasi zote kupitia CCM.

Akiwasilisha mada kuhusu wajibu wa wagombea katika kampeni za Uchaguzi Mkuu Komred Frank Uhaula amesema wagombea ni lazima watambue kuwa malengo ya Chama cha Mapinduzi kuingia katika uchaguzi ni kuhakikisha kinashinda na kushika Dola ili kuendelea kuongoza nchi na kuwatumikia wananchi.

Komredi Uhaula amewakumbusha wagombea wajibu wao katika kampeni na baada ya uchaguzi mkuu ni pamoja na kujitambua kuwa anagombea kupitia CCM hivyo ni lazima kutiii na kufuata maelekezo na miongozo yote ya chama.

Amewasisitiza wagombea hao suala zimanla nidhamu kwa kuwa tabia njema za kiungwana ndanibya chama na katika jamii iliyomzunguka kwa kuwa na ushirikiano na mawasiliano mazuri kama CCM inavyoelekeza.

Komred Uhaula amewasihi wagombea hao kuvunja makundi waliyokuwa nayo kabla ya kuteuliwa na chama, kujenga tabia ya kushiriki katika vikao , semina na mafunzo ya chama pamoja na kuwa kiunganishi kati ya chama na wanachma wa chama cha mapinduzi.

 

Imetolewa na kitengo cha habari (OMPR )

Tarehe 07.09.2025

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.