Kaimu Afisa Mfawi wa Tume za Haki za Binadamu na Utawala Bora THBUB,
Zanzibar Bw. Wilfred Msagati (aliyesimama) akitoa shukurani baada ya kikao na wafanyakazi
wa tume hiyo katika ofisi zao zilizopo Mombasa Wilaya ya Magharibi B Mkoa wa
Mjini Magharibi tarehe 26 Septemba, 2025.
MKURUGENZI Msaidizi
kutoka Idara ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, ya Tume ya Haki za Binadamu
na Utawala Bora (THBUB) sehemu ya Utawala Bora Bw. Mbwana Mussa Mbwana
akizungumza na watumishi wa Tume hiyo Ofisi ya Zanzibar, kwenye ukumbi wa Ofisi
hiyo, Mombasa Wilaya ya Magharibi B, tarehe 26 Septemba, 2025.
Katika nasaha zake, amewahimiza ushirikiano baina yao katika utekelezaji
wa kazi za tume hiyo.
Aidha, amewakumbusha zaidi watumishi hao kujali na kuzingatia muda wa
kuwasili na kuondoka kazini sambamba na kudumisha uadilifu wakiwa kwenye
majukumu yao ya kila siku.
Akizungumzia suala la mavazi Mkurugenzi huyo aliwasisitiza watumishi hao
kuendelea kutii Sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma kwa kuzingatia
mavazi yaliyoainishwa na utumishi wa umma.
Kwa upande wake Kaimu Mfawidhi THBUB ofisi ya Zanzibar ambaye pia ni
Afisa Sheria bw. Wilfred Msagati, amepongeza na ujio wa kiongozi huyuo kwenye
ofisi za Zanzibar na kuahidi kuzifanyia kazi nasaha za kiongozi hiyo kwa
kumuhakikisha uweledi wa tume kutokana na kuongezeka kwa nguvu kazi.
Naye, Mwandishi mwendesha ofisi, bi. Salha Hamza kwa niaba ya watumishi wa Ofisi hiyo walimshukuru Mkurugenzi Mussa kwa nasaha na ushirikiano alioutoa kwa ofisi hiyo. Bw. Mussa alikuwepo ofisi za THBUB Zanazibar kwa ziara ya kikazi.
No comments:
Post a Comment