Habari za Punde

Bumbwini Imeitika Mkutano wa Mgombea Urais wa Zanzibar kwa Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe.Dk.Hussein Mwinyi

Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakijumuika na Msanii wa Kizazi Kipya Yammy (kushoto kwa Rais) akiimba wimbo maalumu wa kupongeza  wa  Uongozi wake Unaoacha alama, wakati wa mkutano wa kampeni yake uliyofanyika katika viwanja vya mpira Bumbwini Mkoa wa Kaskazini Unguja. 
Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakipata picha ya kumbukumbu wakati wa mkutano wa kampeni ya mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliyofanyika katika viwanja vya mpira Bumbwini Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wakishangilia  katika viwanja vya mpira bumbwini wakati wa mkutano wa kampeni ya mgombea Urais wa Zanzibar Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, wakati msanii wa kizazi kipya Yammy akiimba wimbo maalumu wa kupongeza.
Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi, wakati alipowasili katika viwanja vya bumbwini Mkoa wa Kaskazini Unguja, kwa ajili ya mkutano wake wa kampeni ya Urais wa Zanzibar.  
Mwanachama wa Chama cha Mapinduzi akiwa na kipeperushi chenye ujumbe wa Oktoba Tunatiki kwa Dr.Hussein Ali Mwinyi, wakati wa mkutano wa kampeni uliyofanyika katika viwanja vya Bumbwini Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Mkalimali wa lugha ya alama akitowa ishara ya mazungumzo wakati wa mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi uliofanyika katika viwanja vya mpira Bumbwini Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi  wakishereheka wakati wa Kikundi cha Taarab cha Duu wakitowa burudani kwa wimbo maalumu katika viwanja vya mpira Bumbwini Mkoa wa Kaskazini Unguja katika mkutano wa kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.

































No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.