
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Amani Abeid Karume akiagana na mwenyeji wake Waziri wa Usafirishji wa Kenya Chirau Ali Mwakwere katika uwanja wa Ndege wa Kenya jana baada ya kumalizika kwa sherehe za Uzinduzi wa Katiba mpya ya nchi hiyo zilizofanyika katika uwanja wa Uhuru Nairobi Kenya.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume,(kushoto) akikagua gwaride la Jeshi la wanajeshi wa Kenya katika Uwanja wa Ndege wa Nchi hiyo jana alipohudhuria Uzinduzi wa katiba mpya ya Nchi hiyo akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete.Kulia mwenyeji wake Waziri wa Usafirishaji wa Kenya Chirau Ali Mwakwere

Kalonzo Musokya akila kiapo wakati wa sherehe za Uzinduzi wa katika Mpya ya Kenya.

Raila Odinga akila kiapo katika uzinduzi wa katiba mpya ya Kenya wakati a sherehe za uzinduzi wa katiba hiyo zilizofanyika katika uwanja wa Uhuru.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Amani Abeid Karume,(katikati)akiwa na viongozi wengine katika sherehe za Uzinduzi wa Katiba mpya ya Kenya zilizofanyika uwanja wa Uhuru.

Baadhi ya mabalozi na watu mashuhuri walioalikwa katika sherehe za uzinduzi wa katiba mpya ya kenya wakifuatilia kwa makini harakati za uzinduzi zikiendelea.
Picha zote na Ramadhan Othman
No comments:
Post a Comment