Habari za Punde

TUNAWATAKIENI RAMADHAAN NJEMA







Kuna baadhi tayari wameshaanza kufunga leo Jumatano ikiwa ni Ramadhaan ya kwanza na huku nyumbani Zanzibar kwa mujibu wa taarifa ni kwamba mwezi unatarajiwa kutazamwa leo Shaaban 29. Hivyo tunaweza kuanza Ramadhaan kesho Alkhamis tukijaaliwa.

Tunawatakia Waumini wote wa Kiislamu Mfungo wa Ramadhaan utakaokuwa na kheri na baraka na pia kupata dhumuni kuu la kuachiwa huru na moto InshaAllah.

Huu ni mwezi ulioteremshwa Quraan hivyo nasi tujifunge katika kuisoma na kuizingatia hasa ikiwa wasio na mikono hufanya jitihada za ziada kujifunza na kuisoma seuze sisi tuliojaaliwa viungo kamili.
Ramadhaan Mubaarak

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.