Habari za Punde

KITUO CHA ELIMU MBADALA - RAHALEO

Pichani ni baadhi ya vijana wa kike na kiume ambao kwa bahati mbaya na kwa sababu moja au nyengine hawakuwahi kumaliza elimu zao za msingi au sekondari au kutowahi kwenda skuli kabisa enzi za utoto wao. Hata hivyo kwa kuona umuhimu wa elimu wameamua kurudi tena darasani kujiendeleza katika kituo cha Elimu Mbadala jirani na skuli ya Rahaleo.

Hapa husomeshwa masomo tofauti pamoja na masomo ya vitendo yatakayoweza kuwasaidia katika maisha yao.

1 comment:

  1. Mbona wamekaa chini hakuna hata madeksi au mabenchi ya kukalia?

    Ni kuuliza tu

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.