
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk Amani Abeid Karume, akisalimiana na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, baada kufutari pamoja na wananchi wa Mikoa mitatu ya Unguja, futari hiyo iliandaliwa na Rais huko Ikulu ya Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk Amani Abeid Karume,(katikati) akiwa katika futari ya pamoja na wananchi aliyowaandalia huko Ikulu Mjini Zanzibar jana, (kulia) Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha, na (kushoto) Sheikh Khamis Haji Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar.

Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika futari iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk Amani Abeid Karume, kwa mikoa mitatu ya Unguja huko Ikulu mjini Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk Amani Abeid Karume, na Mkewe Mama Shadya Karume, wakisalimiana na wananchi pamoja na kuwashukuru kwa kuweza kufutari nao pamoja jana, katika futari aliyowaandalia wananchi wa mikoa mitatu ya Unguja huko Ikulu Mjini Zanzibar.

Mama Shadya Karume akiwa pamoja na akinamama waliohudhuria katika futari hiyo.
Picha na Ramadhan Othman
No comments:
Post a Comment