Bakar Mussa, Pemba
MGOMBEA Urais wa Zanzibar kupitia chama cha CUF, Seif Sharif Hamad amesema maridhiano ya kisiasa yaliyofikiwa Zanzibar yameleta manufaa makubwa na uchaguzi mkuu wa mwezi ujao utakuwa huru na wa haki.
Hamad alisema nia yake katika kuomba nafasi ya Urais wa Zanzibar ni kutaka kuwatumikia wananchi wa Zanzibar kwa nguvu zake zote na kuleta mabadiliko ya aina mbali mbali kwa maslahi ya wananchi wa Zanzibar.
Mgombea huyo wa Urais kwa tiketi ya CUF, alisema hayo katika mkutano wa hadhara wa chama hicho wa uzinduzi wa kampeni huko kiwanja cha Tibirinzi, Chake Chake Pemba.
Katika mkutano huo, Hamad amewaomba wananchi na wafuasi wa chama hicho kumpa ridhaa yao kuwa Rais ili aweze kuongoza Serikali ya Umoja wa kitaifa na aendelee kuwa pamoja nao kwa kuwatumikia kwa nguvu zake zote.
Seif, alisema iwapo wananchi watampa ridhaa kuwa Rais wa Zanzibar, ataendeleza maridhiano yaliyofikiwa kati ya chama chake na Chama cha Mapinduzi (CCM), chini ya uongozi wa Rais Karume, kwani ana uwezo wa kufanya hivyo.
Alisema Serikali ya Umoja wa kitaifa itakuwa imara na itaongozwa na wananchi wenyewe, na atahakikisha kila mmoja anakuwemo katika Serikali hiyo kwa lengo la kuleta uongozi mwema wenye kujali sheria na haki bila ya ubaguzi wa aina yoyote.
"Hata mwanangu akifanya kosa na vyombo husika vikiamua kuwa nikosa atahukumiwa na akipatikana na hatia atatumikia kifungo", alisema mgombea huyo.
Alieleza kuwa katika serikali atakayoiunda ya umoja wa kitaifa, itakuwa na uwazi na kuziba mianya ya rushwa kwa nguvu zote.
Seif, alisema iwapo wananchi watampa ridhaa ya kuwa Rais, Serikali ya Umoja wa kitaifa, itakuwa inajali misingi ya umoja, kuheshimiana na kuwepo usawa kwa kila mtu.
Maalimu Seif , aliendelea kusema kuwa Serikali yake itahakikisha inaimarisha miundombinu mbali mbali kama vile, barabara, bandari na kuimarisha huduma za afya.

No comments:
Post a Comment