IDADI ya Majaji katika Mahakama Kuu ya Zanzibar imeongezeka kutoka majaji watatu hadi saba, baada ya Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein, kufanya uteuzi huo jana.
Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, walioteuliwa kushika wadhifa huo ni Fatma Hamid Mahmoud, Rabia Hussein Mohamed, Mkussa Isaac Sepetu na Abdulhakim Ameir Issa.
Kati ya majaji hao wapya watatu wa kwanza walikuwa Mahakimu wa Mikoa katika mahakama za Mwera, Mfenesini na Vuga wakati kwa upande wa Jaji Issa alikuwa ni Wakili wa Kujitegemea.
Mahakama hiyo ya Zanzibar ilikuwa na Jaji Mkuu Hamid Mahmoud, Jaji Abraham Mwampashe na Jaji Mshibe Ali Bakari.
Aidha, Dk. Shein amemteua Haroub Sheikh Pandu kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi Zanzibar na alianza kutumikia wadhifa wake huo tangu Novemba 26, mwaka huu.
Kaka hakuna jaji kiongozi zanzibar ! ni jaji mkuu wa zanzibar
ReplyDeleteTumerekebisha Mkuu ahsante kwa kutushtua
ReplyDelete