Habari za Punde

PROFESA MBARAWA AMSHUKURU RAIS KIKWETE

MBUNGE mteule, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, amesema hakuwahi kutarajia kuteuliwa na rais kuwa Mbunge na kuongeza kuwa uteuzi huo uliofanywa Novemba 18 na Rais Jakaya Kikwete, umeonesha kuwa ameheshimiwa na akaahidi kutunza heshima hiyo.

“Sikujua lolote wala sikufikiria kama siku moja ninaweza kuteuliwa na Rais Kikwete kuwa Mbunge katika Bunge la Muungano, ni heshima kubwa kwangu na ninaahidi kuidumisha heshima hiyo,” alisema Profesa Mbarawa.

Akizungumza kwa njia ya simu na gazeti hili Prof Mbarawa ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Tshwane nchini Afrika Kusini alisema ameona kuwa Rais Kikwete amemheshimu.

Akiwa Mhadhiri wa chuo hicho katika Kitivo cha Uhandisi Mitambo, alisema wakati wote alifikiria uzalendo wake ingawa alikuwa nchi ya ugeni jambo lililomsukuma kurudi nyumbani kugombea ubunge katika Jimbo la Mkanyageni, Zanzibar.

Chanzo: Habari Leo

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.