Habari za Punde

DK SHEIN AZINDUA ZAHANATI YA AFYA, KAMBI YA ALI KHAMIS

Na Rajaba Mkasaba, Pemba

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa ufunguzi wa zahanati ya Kambi ya Ali Khamis iliyopo Pemba utasaidia kutekeleza lengo la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar la kuimarisha huduma ya afya nchini.


Hayo aliyasema wakati wa ufunguzi na makabidhiano ya zahanati ya Kambi ya Ali Khamis, iliyopo Mkoa wa Kusini Pemba ambayo imefanyiwa ukarabati mkubwa kwa msaada wa serikali ya Marekani.

Dk. Shein alisema kuwa kituo hicho ni kielelezo madhubuti cha mashirkiano kati ya serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Marekani, ambacho kitashiriki kikamilifu mikakati ya sekali ya kuinua huduma za afya hapa Zanzibar.

Alisema kuwa hatua hiyo inatokana na azma ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964 ambayo pia, yalilenga kuwapatia wanyonge huduma ya afya ambayo kabla ya hpo walikuwa wahaipati.

Alieleza kuwa kabla ya hapo huduma za afya zilikuwa zikitolewa kwa ubaguzi mkubwa na kufanya wengi ya wananchi kukosa huduma hiyo ambapo baada ya Mapinduzi hal hiyo imegeuka na hivi sasa uduma hiyo inatolewa kwa wananchi wote bila ubaguzi.

Katika hotuba yake hiyo, Dk. Shein alisema kuwa huduma za afya kwa hapa Zanzibar zimeimarika kwa kiasi kikubwa ambapo kwa hivi sasa hakuna eneo ambalo linaweza kufikia kilomita tano bila ya kukuta kituo cha afya, Unguja na Pemba.

Alisema kuwa juhudi zinazochukuliwa hivi sasa na serikali ni kuhakikisha mkazo mkubwa unawekwa katika kuinua sekta hiyo ya afya kwa lengo la kuwapa wananchi huduma iliyo bora zaidi na kusisitiza kuwa kituo hicho pia, kitahudumia wananchi.

Akieleza miongoni mwa mikakati iliyowekwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Shein alisema ni pamoja na kuanzisha huduma za upasuaji wa moyo, huduma za figo na maradhi ya saratani hapa hapa Zanzibar badala ya huduma hizo kufuatwa nje ya nchi

Aidha, Dk. Shein alisema kuwa n azma ya serikali kuziongezea nguvu ikiwa ni pamoja na kuongezea wafanyakazi, vifaa na utaalamu wa kisasa hospitali za Wete na Mkoani ili ziwe hospitali za Mkoa

Pia, alisema vituo viwili vya afya ambavyo ni Vitongoji na Micheweni vitapandishwa daraja ili viwe hospitali za Wilaya kwa lengo la kuimarisha huduma hiyo ya afya na kueleza kuwa hatua za serikali kuunga mkono uimarishaji wa huduma za afya Zanzibar n mnasaba wa kufikia lengo hilo.

Pamoja na hayo, Dk. Shein alitoa wito kwa wananchi kutumia fursa ya kuwepo kwa kituo hicho kwa kwenda kuangalia afya zao katika kituo hiho ikiwa ni pamoja na kupima virusi vya ukimwi.

Nae Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Uchum Tanzania, Mhe.Dk. Hussen Mwinyi alisema kuwa kabla ya ukarabati kituo kilikuwa na uwezo wa kutibu wagonjwa takriban 200 kwa mwezi na baada ya ukarabati kituo kina uwezo wa kutibu wagonjwa 600 kwa mwezi.

Pamoja na kutoa matibabu ya magonjwa ya ujumla kituo pia, kinahudumia wagonjwa waloathirika na VVU/UKIMWI.

Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Alfonso Lenhardt naye alieleza lengo la serikali yake la kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika sekta za maendeleo.

Balozi huyo alisema kuwa hospitali hiyo pia,i tatoa huduma kwa akina mama na watoto na kusisitiza kuwa mahusiano mazuri yaliopo kati ya Zanzibar na Marekani yataimarisha zaidi uendelezaji wa miradi ya maendeleo.

Zaidi ya shilingi milioni 200 zimetumika katika ukarabati wa kituo hicho cha afya.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.