Na Juma Mmanga, Dar es Salaam
KIKOSI cha soka cha timu ya Habari Sports, jana kimeanza kwa kutoka suluhu na Redio Kheir katika michuano ya NSSF inayoshirikisha timu za vyombo vya habari.
Katika pambano hilo la kundi B lililofanyika kwenye uwanja wa TCC Chang’ombe, wanaume hao licha ya kushambuliana kwa nguvu, walishindwa kuweka mpira nyavuni na kulazimika kugawana pointi moja moja.
Katika mechi nyengine za mashindano hayo, matokeo kama hayo ya sare tasa yalijiri pia kwenye mechi kati ya Jambo Leo na TBC, huku Uhuru na Mwananchi zikienda sare ya kufungana bao 1-1.
Leo itakuwa zamu ya Mlimani kuoneshana kazi na Changamoto, wakati Global itakuwa kazini dhidi ya New Habari.
Habari itarudi tena dimbani Machi 25 kwa kumenyana na Global
No comments:
Post a Comment