Habari za Punde

KIZIMBANI KWA KUKUTWA NA DAWA ZA KULEVYA

Na Mwanajuma Said

MAHAKAMA ya Wilaya Mwera, imemtaka mtuhumiwa anayedaiwa kupatikana na bangi, Omar Khamis (36), Mkaazi wa Mwanakwerekwe Mjini Unguja, kutojibu lolote baada ya kusomewa shitaka hilo mahakamani.

Uamuzi huo wa Hakimu wa Wilaya, Hussein Makame, ulikuja kutokana na kesi hiyo husika kuwa ya mahakama ya Mkao, mbele ya Hakimu Faraji Shomari Juma.

Awali akisoma shitaka hilo, Mwendesha Mashitaka wa Polisi Inspekta Saidi Mbwana aliifahamisha mahakama kuwa kosa la upatikanaji wa bangi ni kinyume na kifungu 16 (1)(b) cha sheria namba 9/2009 ya sheria ya kuzuia dawa ya kulevya Zanzibar.

Hati hiyo ya mashitaka ilieleza kuwa mtuhumiwa huyo alipatikana na kifurushi kimoja cha bangi ndani ya mfuko wake wa suruali ikiwa na uzito wa gram 1.175.

Kwa mujibu wa hati hiyo, tukio hilo lilitokea Nyarugusu Wilaya ya Magharib Unguja, saa 2:00 usiku April 1 mwaka huu.

Mara baada ya kusomewa madai hayo, mtuhumiwa hakutakiwa kujibu chochote kutokana na kesi hiyo kuwa ni ya mahakama ya Mkoa na kuamuriwa kwenda rumande hadi April 20 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.