Habari za Punde

RASIMU YA KATIBA YACHANWA



Salma Said, Zanzibar .

MKUTANO wa kutoa maoni kuhusu mswaada wa uundwaji wa kamisheni ya kukusanya maoni kuhusu katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umevunjika hapa rasimu za mswaada huo kuchanwachanwa katika mkutano huo.

Kiongozi wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar, Sheikh Farid Hadi Ahmed akiongea katika mkutano huo uliofanyika ukumbi wa shule ya Haile Sellasie ndio aliyechana mswaada huo na kufuatiwa na watu wengine kuchana nyaraka hizo kwa madai kwamba hauna maslahi ya wazanzibari na kwamba suala hilo halijazingatia hadhi ya Zanzibar hivyo hauna faida kwa wananchi.

“Huu mswaada mnautaka? Hatuutaki huu mswaada mnautaka? Hatuutak…huu mswaada mnautaka? Hatuutaki. Mwenyekiti na waheshimiwa mnasubiri nini tena basi kama mnataka tuoneshe kivitendo hatuutaki basi ndio hivi..” akachanachana mswaada huo huku wengine wote wakaendelea kuchanachana nyaraka walizokuwa nazo.

Mkutano huo ulipangwa kumalizika saa nane mchana lakini ilipofika saa saba Sheikh Farid alisema hakuna haja ya kuendelea na mkutano huo huku badhi ya wananchi wakiwataka wananchi wengine kundoka katika mkutano huo kwa kuwa hakuna faida a kujadili kitu ambacho haina faida kwao.

Awali akiochangia mjadala huo Sheikh Farid alisema alijaribu kufutalia mchakati mzima wa rasimu hiyo ya katiba lakini inaonesha kwamba kuna taratibu nyingi hazikufuatwa na hivyo hakuna sababu ya kuendelea kuujadili kwa kuwa hauna maana.

“Hapa tumesikia kelele nyingi sana kwa hivyo ilikuwa inatosha tutawanyike kabisa, tunakwenda katika kujadili marekebisho ya katiba ya Tanzania lakini swali jee katiba ya Tanganyika mnao? Jee hapa huo muungano uko wapi? Kipi cha kutangulizwa? Kwanza kafanyeni katiba ya Tanganyika kwanza” alisema huku akishangiriwa na wananchi.

“Mswaada kwao sisi hatuna shida ya kutungiwa mswaada basi tunasema hatuutaki kuvundwa vundwa….huu mswaada mnautaka… hamuutaki? Aliwauliza wananchi na kujibiwa hatuutaki….mnasubiri nini chengine mkitaka muone kivitendo kwamba hatuutaki basi ndio hivi” alisema Sheikh Farid huku akichana chana mswaada huo.

Akichangia kwa ufupi mswaada huo Sheikh Farid amesema lazima maamuzi ya wananchi yachukuliwe na suala la kuheshimu mawazo yao ni suala la lazima hivyo hakuna sababu ya kuwalazimisha kitu wasichokitaka.

“Natoa wasia wangu kwa serikali ya mapinduzi na serikali ya umoja wa kitaifa tunataka kura ya maoni tuulizwe muungano tunautaka au hatuutaki” alisema huku akipigiwa makofi kwamba muungano huo hatuutaki” alisema.

Kufuatia kutofautiana kati ya uongozi wa meza kuu na wananchi wanaosikilizwa maoni yao , Mwenyekiti wa kamati ya katiba na sheria ya bunge la jamhuri ya muungano Jadi Simai Jadi alisema alilazimika kuvunja kikao hicho na kuwataka wananchi waondoke kwa salama kwa kuwa hali ya usalama ingeweza kutoweka sehemu hiyo wakati wowote.

“Sasa mkutano wetu utakuwa umemalizia hapa maana naona hali ya usalama inaweza kutoweka kwa hivyo niseme kwamba tunafunga mkutano huu” alisema Simai huku kelele ya wananchi zikiwa zimesambaa hadi nje wakiimba muungano hatuutaki.

Hata hivyo baadhi ya askari waliokuwepo pale walikuwa wakizunguka zunguka lakini wananchi waliondoka kwa usalama bila ya purukushani lakini wameondoka na wimbo wakiimba kwa sauti kwamba hawautaki muungano na kuitaka serikali kuitisha kura ya maoni haraka juu ya kuulizwa iwapo wanataka kendelea na muungano au laa.

“Muungano hatuutaki muungano hatuutaki ….tunataka kura ya maoni tunataka kura ya maoni” alikuwa wakiimba baadhi ya wananchi huku wengine wakiwa wamebeba makaratasi yalioandikwa hatutaki muungano.

Wakati wote ukumbi ulikuwa umetulia huku mwendeshaji wa mjadala huo ambaye alitoa maelezo kwa ufupi Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Samuel Sitta pamoja na Waziri wa Nchi ofisi ya Makamo wa kwanza wa rais Muungano Samia Suluhu Hassan waliwaomba wananchi kutoa maoni yao kwa utaratibu mzuri bila ya jazba na wanaruhusiwa kuzungumzia suala la muungano tofauti na mkutano wao wa juzi ambapo wananchi waliambiwa wasigusie suala la muungano jambo ambalo lilizusha zogo kubwa katika ukumbi huo..

Akiongea katika mjadala huo juzi jioni Muasisi wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Mzee Hassan Nassor Moyo ambaye alikuwa waziri wa sheria na katiba huo wa kuunganishwa nchi mbili na kuwa Muungano alisema yeye amekuwa shahidi wa makubaliano hayo kati ya Zanzibar na Tanganyika ha hakuna asichokifahamu kuhusiana na makubaliano hayo huku akitaka suala la wananchi kupewa uhuru wa kujadili muungano wao lipewe nafasi kubwa.

“Mnatwambia tusizungumze suala la muungano mnataka tuzungumze nini hapa wakati hilo ndio jambo la msingi….mnataka tuzungumze nini? …hili ndio jambo tutakalolizuingumza” alisema huku akisisitiza kwamba kosa walilolifanya wakati huo la kupitisha maamuzi bila ya kuwashirikisha wananchi lisirudiwe tena hivi sasa kwa kuzingatia vijana wa leo wamesoma na sio wajinga kama wao.

Aidha aliongeza kwamba “Nilikuwa waziri wa sheria wakati huo mambo haya ni 11 lakini hivi sasa yameongezeka naambiwa yamefikia mpaka 30 haya yote yaliongezwa na wenzetu bara ….na kwa yale yalioengezwa na watu wa unguja Jumbe alifukuzwa kazi sasa spirit ile ile ya Jumbe ipo maana sisi wengine tuhai hatujafa na pia wapo wanaunga mkono na yeye mwenyewe jumbe hajafa yuhai””alisema Mzee moyo huku akionesha nakala ya makubaliano hayo ya muungano.

Alisema mambo waliyofanya miaka iliopita wakati wa kina Lusinde, Hassan Moyo na Sitta, hivi sasa hayapo tena na wasizuie kuwapo kwa mabadiliko kwani kazi yao imekwisha na watafanya makosa kuzuia mambo ya Muungano Wazanzibari waasiyajadili katika katika mpya.

“Haiwezekani hata kidogo wapewe nafasi waseme kwani hili nalisema ndani ya moyo wangu Nyerere alikuja Zanzibar na karatasi ina mambo 11, mimi nilikuwa Waziri wa Sheria alinipa faili na hakuna hata sentesi moja iliotolewa leo tunaambiwa kuna mambo 22 na Jumbe alipotaka kuengeza alifukuzwa kazi, sasa mnaposema tusizungumze mambo ya Muungano maana yake nini mnawaambia nini Wazanzibari”,alisema Mzee Moyo.

Mzee Moyo ambaye alikuja hapo na hati za makubaliano ya Muungano alisema mambo waliokuwa wameafikiana Nyerere na Mzee Karume wakati huo yameweza kuheshimiwa na viongozi wengine kulingana na wakati lakini kwa sasa vijana hawawezi kupangiwa mambo kama ilivyokuwa huko nyuma ambapo sas vijana wanahitaji kurekebisha na kuwepo muundo wanaoutaka wao jambo ambalo alisema lazima serikali iwasikilize wananchi.

“Tusiwazuwie vijana hawa kufanya muungano wanaoutaka wao wenyewe, mimi na karume na jumbe tumeufikisha hapa …na haiwezekani kama tumeshaufikisha hapa halafu tuendelee hivi hivi bila ya wao vijana kuwaachia wenyewe wanavyotaka kuuendeleza lazima tukubali kuwapa fursa waseme wenyewe wanataka muungano wa aina gani …tusiwazuwia wenyewe …sisi yetu tumeshwikwisha” alisema Mzee Moyo.

Mzee moyo alisikitishwa na tabia ya kuambiwa kwamba suala la muungano zilijadiliwe jambo ambalo amesema iwapo halitazungumzwa kutakuwa hakuna jembo jengine la kulijadilia zaidi ya muungano kwa kuwa ndio kubwa kwa Zanzibar .

Akizungumza katika mjadala huo, Waziri wa Katiba na Sheria, Abubakar Khamis Bakari alisema utaratibu uliotumiwa sio na serikali haikushirikishwa katika uandaaji wa rasimu hiyo na serikali ya muungano haifajafan ya uungwana hata kidogo.

Alisema licha ya kuwa hawajashirikishwa lakini serikali ya Zanzibar kupitia mwanasheria mkuu wake aliandika barua kupeleka serikali ya muungano lakini hakujibiwa angaua kwamba barua yao imepokelewa lakini pia walipeleka mapendekezo yao 14 lakini jambo la kusikitisha ni mambo mawili tu ndio yalioingizwa katika rasimu hiyo na badala yake kuongezwa mambo mengine manane kinyume na makubaliano.

Aidha Mzee Moyo alisikiyishwa kusikia Mwanasheria wa Zanzibar kueleza kuwa hana taarifa ya mswada huo jambo ambalo ni la maajabu kwa serikali kwani kinachotengenezwa ni katiba mpya na sio kutia viraka na ni vyema kamati hiyo ikapeleka ujumbe wa Wazanzibari nini wanachotaka.

“Mnasema tusiseme mnataka tuzungumze utumbo, lazima mabadiliko yafanywe kwani hivi sasa vijana wamesoma na hawakubali kuamuliwa, Nyerere alikuwa anakubaliana na mzee Karume hakua anatoa maamuzi, Wewe sita umefanya kazi na Nyerere, Jumbe na Karume msifanye mambo ya wakati ule ‘is over’ ”, alimalizia Mzee Moyo na kuafuatwa na nyimbo katika ukumi zima zikiimbwa “sisi sote tumegomboka kwa ndugu zetu walopotea ,,,,walooooo walopigania nchi yetu makusudi ..makusudi ya kutukomboa na sisi.. na sisi hatutorud nyuma sote mbele sote mbele tutaendeleaaaaaa” .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.