Na Khamisuu Abdalla
MUHANDISI Mkuu Idara ya Ujenzi na Utunzaji Barabara Zanzibar, Mbarouk Juma Mbarouk amesema nyumba ambazo zinatarajiwa kuvunjwa kupisha ujenzi wa Barabara ya Darajabovu ziyalipwa fidia.
Akizungumza na muandishi wa habari hizi huko ofisini kwake Saateni, mkuu huyo alisema kabla ya Idara kutoa shauri hilo katika kikao, waliamua nyumba ambazo zilijengwa mapema lazima zilipwe ili kuondosha migongano baina ya wananchi na Idara hiyo.
Alisema tathmini ya kuwalipa watu hao watakaobomolewa nyumba zao tayari imepelekwa serikalini, ambapo serikali ipo katika hatua ya kuwalipa fidia ya kuanza kwa kazi ya ubomoaji wa nyumba hizo.
Aidha Mbarouk alifahamisha kuwa endapo atatokea mtu yoyote atajenga kwa kutofuata taratibu mtu huyo hatolipwa fidia yoyote.
Alisema kuwa kumekuwa na baadhi ya wajanja wanapolipwa fidia huwauzia watu wengine nyumba hizo na kupelekea kuitia ubayani serikali na kudai huwajalipwa fidia zao.
"Kumekuwa na baadhi ya watu wanapolipwa fidia huwauzia watu wengine nyumba zao na kupelekea kuitia ubaya serekali na kudai hawajalipwa fidia zao alisema mkuu huyo"
Hata hivyo Muhandisi huyo alisema kuwa nyumba hizo zitakazobomolewa zitalipwa kutokana na thamani ya nyumba yenyewe ilivyo.
Aidha aliwataka wananchi kutokujenga nyumba karibu sana na Barabara ni hatari kwani huwafanya watu wanaopita kwa miguu kupita barabarani na kusababisha hasara ya kuvunjiwa nyumba zao.
Gharama za ujenzi wa Barabara ya Darajabovu zinatarajiwa kufikia bilioni tatu na itachukuwa muda wa miezi mitano.
No comments:
Post a Comment