Habari za Punde

BALOZI SEIF AKUTANA NA WAZIRI WA AFYA WA MAREKANI

Ugonjwa wa Malaria ndio uliyokuwa ukiongoza kwa kuuwa watu wengi katika Visiwa vya Zanzibar miaka michache iliyopita kabla ya kuanza mradi wa Kataa Malaria hapa nchini.


 Hayo yalielezwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Balozi Seif Ali Iddi katika mazungumzo yake na Waziri wa Afya wa Marekani Mhe Kathelin Sebelius aliyefika na ujumbe wake Ofisini Vuga kusalimiana naye.

 Mheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais alisema maradhi ya Malaria yamepungua sana kutoka asilimia zaidi ya 40 hadi sasa chini ya asilimia moja na jitihada zinaendelea za kuzuwia ongezeko la maradhi hayo kwa kutumia vyandarua na kupiga dawa majumbani.

 Kuhusu tatizo la upungufu wa madaktari Mhe Balozi alisema Serikli ya Mapinduzi ya Zanzibar imefanya juhudi kubwa za kusomesha madaktari wazalendo ndani na nje ya nchi, lakini jitihada hizo zina kwamishwa na umasikini kwa kuwa madaktari hufuata maslahi bora nje ya nchi.

 Kwa upande wake Waziri wa Afya Mhe Juma Duni Haji alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Saba imekusudia kulitatua tatizo la kukimbia madaktari na wataalamu kwa kuwapa maslahi bora yanayokaribiana na Tanzania Bara ili yaonekane sawa ikijumuishwa na faida ya kuwa nyummbani.

 Naye Waziri wa Afya wa Marekani Mhe Kathelin Sebelius alielezea fursa aliyopata ya kutembelea miradi ya Afya iliyosaidiwa na Marekani na kupongeza maafikiano yaliofikiwa ya kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa na uendeshaji wake wenye tija.

 Alisema mafanikio hayo ni mfano mzuri kwa mataifa mengine yenye migogoro katika kutafuta njia bora ya usuluhishi migogoro yao bila ya kuingiliwa na wasuluhishaji wa nje

Akizungumzia sula la madawa ya Kulevya Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe Fatma Abdulhabibi Fereji alisema uchache wa vituo vya kuhudumia waathirika wa madawa hayo na vifaa vyake ni moja ya matatizo yanayozikabili jitihada zao za kupambana na janga hilo.

 Alisema vituo hivyo vinamsaada mkubwa kwa vile waathirika hao huviamini zaidi kuliko Hospitali kwa kuwapatia tiba na huduma nyengine za afya, jambao ambalo huiwezesha Serikali kupata taarifa zao na kutoa nasaha bila ya taabu.

 Hatimaye Mhe Makamu wa Pili wa Rais na Waziri huyo wa Afya walipeana zawadi ikiwa ni kama kumbu kumbu za mazungumzo yao.  


Abdulla A. Abdulla


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.