Na Mwantanga Ame
JAMII imeshauriwa kuacha kuwafanyia vitendo viovu watoto waenye ulemavu baada ya kuibainika badhi ya watu wamejitayarisha kuwaharibu kimaisha.
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais, Mama Asha Seif Iddi, aliyasema hayo jana wakati akishiriki katika ufunguzi wa tamasha la Michezo kwa watoto wenye ulemavu lilofanyika katika viwanja vya Bustani ya Jamhuri Mjini Zanzibar.
Mama Asha, alisema inasikitisha kuwa baadhi ya watu wameamua kuwaingiza watoto wenye ulemavu kwa kuwafanyia mambo maovu yakiwemo ya kuwapa ujauzito ama kuwabaka, jambo ambalo linawavunjia haki zao za kimsingi.
Alisema jamii inapaswa kuzingatia kuwa ulemavu wanapatiwa matunzo mazuri kama makazi, masomo na mambo mengine yanayoweza kuwajengea hatma njema baadae.
Alisema vitendo hivyo havilingani na ubinadamu ambao unataka kila mtu apewe hshima yake na haki ya kuamua atakalo na siyo kulazimishwa.
Alisema serikali ya Zanzibar mara zote imekuwa ikitoa kipaumbele cha kupewa haki watoto wenye ulemavu na wengine bila jamii kuwapuuza.
Hata hivyo, Mama Asha, aliwataka baadhi ya wazazi ambao bado wamekuwa na tabia ya kuwaficha watoto wenye ulemavu kuacha mchezo huo na badala yake wawajumuishe katika vituo vya Walemavu ili waweze kujua haki zao.
Alisema kuendeleza tabia hiyo kunaweza kuwafanya watoto hao kukosa elimu wakati wengi wao wamekuwa wanaonekana kuwa bado wana uwezo wa kusoma na kuandika.
Katika kufanikisha sherehe hiyo, Mama Asha aliwakabidhi fedha kwa ajili ya kufanikisha tamasha hilo ambapo watoto hao wanatarajiwa kutembezwa sehemu mbali mbali za vivutio na kumbukumbu ya Zanzibar.
Mapema Mwakilishi wa mkurugenzi wa Jumuiya ya watu wenyewe Ulemavu Zanzibar, Ali Abeid, akitoa maelezo yake alisema dhamira ya tamasha hilo kuona inawajengea mazingira ya watoto wa aina hiyo kuvifikia
viwanja vya kufurahia watoto.
No comments:
Post a Comment