Habari za Punde

RAIS KIKWETE AFUTARISHA WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU KATIKA VIWANJA VYA IKULU ZANZIBAR.


 RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzin Dk.Ali Mohamed Shein, wakijumuika katika Futari ilioandaliwa na Rais wa Tanzania Dk.Kikwete katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd na Naibu Kadhi wa Zanzibar Khamis Haji Khamis wakijumuika katika waumini wa dini ya Kiislam katika futari hiyo viwanja vya Ikulu. 

 WANANCHI wakijipatia futari ilioandaliwa na Rais wa Tanzania Dk Kikwete kwa Wananchi wa Zanzibar iliofanyika viwanja vya Ikulu Zanzibar.

WAUMINI wa dini ya Kiislam wakijipatia futari maalum ilioandaliwa na Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete kwa waumini katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani unaotarajiwa kumalizika wiki ijayo.   

 WAUMINI wa Kiislam wakifuturu katika viwanja vya Ikulu Zanzibar, katika futari ilioandaliwa na Rais wa Tanzania. 

 RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete wa tatu,kulia Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd na kushoto Naibu Kadhi wa Zanzibar Khamis Haji Khamis, Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho wakimsikiliza Sheikh Soranga akitowa shukrani katika hafla hiyo ya futari katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.


 MKE wa Rais wa Tanzania Mama Salma Kikwete , Mama Mwanamwema Shein, Mama Asha Balozi Seif Idd, wakiitikia duwa inayosomwa na Sheikh Fadhili Soraga baada ya kumaliza futari.    

RAIS Kikwete akisalimiana na Mama Fatma Karume katika viwanja vya Ikulu Zanzibar baada ya kumaliza kufutari.  
 MKE wa Rais wa Tanzania Mama Salma Kikwete akisalimiana na Wananchi  baada ya kumaliza futari ilioandaliwa na Rais Kikwete iliofanyika viwanja vya Ikulu Zanzibar.


MKE wa Rais wa ZanzibarMama Mwanamwema Shein akiwa  na Wake wa Makamu wa Pili wa  Rais wa Zanzibar, Mama Asha (katikati) na Mama Pili, kushoto
MKE wa Rais wa Tanzania Mama Salma Kikwete na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein wakiwa katika viwanja vya Ikulu Zanzibar baada ya kumaliza kufutari wakitoka katika viwanja huvyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.