Imeelezwa kwamba walimu katika madrasa za Quraan Visiwani Zanzibar wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha kutokana na baadhi ya wazazi kushindwa kutoa ushirikiano.
Akizungumza katika Mashindando ya kuhifadhi kitabu kitukufu cha Quraan yaliyofanyika katika msikiti wa Mahonda jana, Sheikh Omar Fadhil alisema wazazi wana wajibu wa kutoa michango ya hali na mali kwa walimu hao katika kuendeleza masomo ya watoto wao.
“Kwa hakika walimu wetu wa Madrasa wamekuwa wakipata usumbufu na baadhi ya wakati kukata tamaa, hawalipwi mshahara wala posho, wanategemea sana michango kutoka kwa wazazi au walezi ambao wengi wao wamekuwa hawachangii chochote” Alisema Sheikh Fadhil.
Sheikh Fadhil alisikitishwa na ugumu wa maisha unawakumba walimu hao na kutoa wito kwa jamii kuwasaidia kwani wamekuwa wakitoa mafunzo ya kiimani kwa watoto hapa nchini.
Alisema Walimu wengi wa Madrasa wamekua na maisha duni kutokana na baadhi ya wazee kutowathamini na kutojali kazi yao jambo ambalo linasababisha kuwa na wakati mgumu wa kutoa mafunzo kwa vijana.
Katika hatua nyengine, Sheikh huyo amewakumbusha waumini wa dini ya Kiislamu kutenga muda wao katika kusoma kitabu cha Quraan ambacho kina mafunzo mengi kwa wanaozingatia.
“Ndugu zangu Waislamu, tumetakiwa tusome Quraan mara kwa mara… hivyo nawakumbusha waumini wenzangu ni vizuri tukaongeza bidii katika kusoma hasa mwezi kama huu wa Ramadhaan” Aliwakumbusha Sheikh Fadhil.
Mwalimu wa Shule ya Sekondari Kiponda, Said Bakari akizungumza katika mashindano hayo aliwakumbusha wazazi kuwa makini na watoto wao wakati wa sikukuu ya Idd el fitr.
Alisema ilivyo kuwa asilimia kubwa ya watu wa Zanzibar ni waumini wa dini ya kiislamu, kuna kila sababu kwa wazazi kuwasisitiza watoto wao kufuata maadili ya dini hiyo.
Katika mashindano hayo washindi wa kwanza walikuwa ni Mariam Ali aliyehifadhi juzuu 15 , Khamis aliyehifadhi Juzuu 7, Ibrahmu aliyehifadhi juzuu 5, Ayoub Kassim amehifadhi juzuu 3, Asya Kassim amehifadhi juzuu 2, Abdulrahman Suleimani amehifadhi juzuu 1 na juzuu 1 Kassim Suleiman.
Mashindano hayo ya kuhifadhi Quran yalishirikisha jumla ya Madrasa 15 za Vijiji vya Mkataleni na Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja
Hali ya walimu wa mardassa kweli ni ngumu lkn na wao wanatakiwa wabadilike,wengi wao hawana taaluma ya kufundisha kur'ani vizuri, ukitoa kujua kusoma wao wenyewe,Pili hawawahimizi wanafunzi wao kutoa kipaombele pia kwenye masomo ya skuli mfano wanaofanya mitihani ya shule hawapunguziwi muda wa kwenda madrassa au kutiwa moyo na kupongezwa na maustadhi wao wanapo faulu na kwa namna hiyo dogo akifaulu na kupata kazi hamjui ustadhi,hasaidii wala kupita ten madrassa tatu,wanafunzi wa level tofauti wanachanganywa pamoja hujui alie mbele wala nyuma kelele tu!na akitokea ustadhi mwenye taaluma nzuri na aliekwenda skuli wallahi hafi njaa,watu wote watapeleka watoto wao huko na watalipa! kusomesha kurani ni kazi kama zilivyo kazi nyingine na si kweli kua kupokea mshahara kwa walimu wa madrassa ni dhambi! hivi kweli mzazi ajue kuna madrassa inayofundisha vizuri mfano kabla mtoto hajaingia sekondari kesha hitimu mtu asilipe..subutu!! hata 50,000 kwa mwezi.
ReplyDelete