Habari za Punde

MAZIKO YA MWANDISHI WA HABARI MKONGWE MAULID HAMAD MAULID.



 WANANCHI waliohudhuria mazishi ya Maulid Hamad wakiitikia duwa baada ya kusoma hitma katika Msikiti Noor Mahmmed Mombasa kwa Mchina.
 SWALA ya maiti ikiongozwa na Sheikh Othman Maalim wakiusalia mwili wa marehemu Maulid Hamad katika Masjid Noor Mahammed Mombasa kwa Mchina, 



 MSAFARA wa magari yakielekea Bumbwini Msufini yakiwa katika barabara ya Bumbwini.



 WADAU wa michezo Zanzibar wakihuhudhuria mazishi wa Mwanahabari wa siku nyingi Zanzibar na mwanamichezo wa Timu ya Taifa ya Jangombe Mkombozi wa Ngombu Maulid Hamad.
 WAKURUGENZI wa Vyombo vya Habari vya Coconut Fm na Hit Fm na Zanzibar Cable wakitafakari juu ya kifo cha Mfanyakazi wao alikuwa akivitumikia vyombo hivyo kwa kutowa habari mbalimbali.

 WANANCHI wakihudhuria mazishi ya mwandishi wa habari wa vyombo vya ITV na Redio One wakiwa na huzuni kwa kuondokewa na mpiganaji wa haki za wanyonge kupitia kalamu yake. marehemu Maulid Hamad.Mungu amlaze pema peponi amin.    
 MKUU wa Utawala wa ITV na Redio One Ayub Semvua akiwakilisha Wafanyakazi akitowa salamu za rambimrambi kwa Wanafamilia wa marehemu mMaulid Hamad baada ya kumaliza kuzikwa huko Kijijini kwao Bumbwini Msufini. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.