Habari za Punde

STAR TIMES ILIPOKABIDHIWA LESENI LEO

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad katikati waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Viongozi wa Kampuni ya Star Times ya China baada ya makabidhiano ya Leseni kwa Kampuni hiyo katika sherehe zilizofanyika leo Hoteli ya Zanzibar Beach Resort.

Mkurugenzi wa Mipango wa Wizara ya Habari Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar Joseph Kilange akimkabidhi Mwenyekiti wa Kampuni ya Star Times ya China Pang Xin Xing Leseni Kampuni hiyo kufanya kazi zake rasmi Zanzibar katika sherehe iliyofanyika leo Hoteli ya Zanzibar Beach Resort.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad alipokuwa akitoa hotuba katika Sherehe ya kukabidhiwa Leseni Kampuni ya Star Times ya China kufanya kazi Zanzibar iliyofanyika leo Hoteli ya Zanzibar Beach Resort.

Mwenyekiti wa Kampuni ya Star Times ya China Pang Xin Xing akitoa hotuba ndogo katika Sherehe ya kukabidhiwa Leseni Kampuni hiyo kufanya kazi Zanzibar iliyofanyika leo Hoteli ya Zanzibar Beach Resort.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akitia saini Kitabu cha Wageni kabla ya tukio la kukabidhi Leseni Kampuni ya Star Times ya China leo katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort kulia ni Naibu Waziri wa Redio, Televisheni na Filamu wa China Li Wei
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad alipokuwa na mazungumzo na Naibu Waziri wa Redio Televisheni na Filamu wa China Li Wei wa mwisho kuliani kwake kabla ya Sherehe ya kukabidhiwa Leseni Kampuni ya Star Times ya China kufanya kazi Zanzibar iliyofanyika leo Hoteli ya Zanzibar Beach Resort.


PICHA ZOTE NA Hamad Hijja - Maelezo Zanzibar

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.