Habari za Punde

SHEREHE ZA KUWAPONGEZA MBUNGE NA MWAKILISHI WA JIMBO LA AMANI.

 Mkurugenzi wa Idara ya Elimu Msingi na Maandalizi Mwalimu Uled , akimkabidhi Cheti Mwakilishi wa Jimbo la Amani Mwalim Mussa Hassan, kwa mchango wake katika Elimu Jimboni humo.Sherehe hizo zimefanyika katika viwanja vya Skuli ya Kilimahewa.

Mkurugenzi wa Idara ya Elimu Msingi na Maandalizi Mwalimu Uled , akimkabidhi Cheti Mwakilishi wa Jimbo la Amani Fatma Mbarouk Said, kwa mchango wake katika Elimu Jimboni humo.Sherehe hizo zimefanyika katika viwanja vya Skuli ya Kilimahewa. 
 Mbunge wa Jimbo la Amani Mwalim Mussa Hassan, akizungumza na Walimu wa Skuli za Kilimahewa A,B na Skuli ya Sebleni ambazo ziko katika Jimbo la Amani,akitowa nasaha zake kwa walimu hao kwa jitihada zao kuwawezesha wanafanzi wao kufanya vizuri katika mitihani ya iliombalizika hivi karibuni, na kuahidi kuazisha darasa kwa Wanafunzi ambao hawakubahatika kupasi, kuingia kidatu cha Tatu, ili kuhakikisha wanafanya vizuri na kuendelea na masomo yao juu.
 Walimu wa Skuli za Jimbo la Amani wakimsikiliza Mbunge na Mwakilishi wa jimbo hilo, katika sherehe za kuwakabidhi Vyeti kwa mchango wao jimboni, sherehe hizo zimefanyika katika viwanja vya Skuli ya Kilimahewa.   
 Mwakilishi wa Jim,bo la Amani Fatma Mbarouk Said,akitowa shukrani zake na nasaha kwa Walimu katika jitihada zao za kutowa elimu, kwa wanafunzi wa jimbo la Amani , katika sherehe za kuwapongeza Mbunge na Mwakilishi kwa mchango wao katika jimbo hilo kuimarisha Elimu na kuwahamasisha Wanafunzi kufanya vizuri masomo yao. 
 Walimu wakiwa makini kusikiliza nasaha za Viongozi wa Jimbo katika Tfrija ya kuwatunuku Vyeti Mbunge na Mwakilishi kwa mchango wao katika Elimu, wakihakikisha wanafunzi wa jimbo hilo wanafanya vizuri katika mitihani yao. 
 Mwenyekiti wa Kamati ya Skuli za Jimbo la Amani,Abdalla Ali Vuai, akizungumza katika tafrija hiyo jinsi kamati yake inavyoendeleza maendeleo ya watoto kupsata Elimu na kufaulu katika Mitihani yao,    
 Mkurugenzi wa Idara ya Elimu  Maandalizi na Msingi, Mwalim Uled, akitowa shukrani kwa Waheshimiwa kwa ushirikiano wao na Walimu katika kufanikisha kuwaandaa Wanafunzi kwa ajili ya mitihani yao ya Darasa la Saba na Kidatu cha Pili. 
Mwl. Ramadhani Sadifa, akisoma risala kwa niaba ya Walimu wa skuli tatu za Jimbo la Amani kwa Waheshimiwa, katika tfrija ya sherehe za kuwapongeza zilizofanyika Skuli ya Kilimahewa.     
Walimu wa Skuli za Jimbo la Amani Kilimahewa A,B na wa Skuli ya Sebleni, wakimsikiliza Mbunge akitowa nasaha zake na pongezo kwa Walimu kwa jitihada zao.    
 Waheshimiwa na meza Kuu wakitikia dua, baada ya kutowa nasaha zao kwa Walimu ya Skuli za Jimbo la Amani.  
Mwalim Rajab Othman, akisoma Dua baada ya kumalizika kwa sherehe za kuwatunuku Vyeti Mbunge na Mwakilishi kwa mchango wao katika nyanja ya Elimu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.