Habari za Punde

Maalim Seif Awataka Watendaji CUF Kuwa Karibu na Wanachama

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na Mkurugenzi wa habari na haki za binadamu wa Chama hicho Salim Bimani baada ya kuwasili katika hoteli ya Mazsons Mjini Zanzibar kwa ajili ya kufungua semina elekezi kwa wenyeviti na makatibu wa wilaya wa CUF. Katikati ni mwakilishi wa Jimbo la mgogoni Pemba Aboubakar Khamis Bakar.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad akielekea ukumbi wa mkutano katika hoteli ya Mazsons Mjini Zanzibar kwa ajili ya kufungua semina elekezi kwa wenyeviti na makatibu wa wilaya wa CUF. (Picha, Salmin Said, OMKR)

Na Hassan Hamad (OMKR).

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad amewataka watendaji wa chama hicho ngazi ya wilaya kufanya kazi kwa karibu na wanachama ikiwa ni hatua muhimu katika kukijenga chama chao.

Amesema watendaji hao wana nafasi kubwa katika kukijenga na kukiimarisha chama hicho, ikizingatiwa kuwa wao ndio wenye mawasilianao ya karibu zaidi na wanachama pamoja na wananchi kwa ujumla.


Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ametoa changamoto hiyo leo huko hoteli ya Mazsons Shangani mjini Zanzibar, alipokuwa akifungua semina elekezi kwa wenyeviti na makatibu wa wilaya wa chama hicho, yenye lengo la kujadili juu ya dhana ya utumishi wa umma.

Amewataka wajumbe wa mkutano huo kuijadili dhana hiyo kwa umakini mkubwa, kwa kuzingatia zaidi maslahi na maendeleo ya chama hicho, sambamba na kuhimiza suala la uwajibikaji kwa viongozi wa ngazi zote za chama.

Semina hiyo imehudhuriwa na viongozi mbali mbali wa chama hicho wakiwemo wenyeviti na makatibu wa wilaya kutoka wilaya zote za Unguja na Pemba.


3 comments:

  1. Ndio mzee,.. naona ngangarii!
    Mnakweda kufkuza wengine nin?

    Kwakeli sipati picha, watu wamejenga chama kwa gharama kubwa ya mali na damu hatimae wanakuja kukiua kienyeji?

    Huku wakijenga hoja eti kuna usaliti!,..usaliti usizuke enzi za 'melody' uje uzuke leo..wakati kuna kula?..watu wanajua kudanganywa wallah!

    Wengine wanakwenda mbali zaidi kwa kudai eti watu wa bara hawaaminiki, wakati wana wabunge wawili bara jambo lililowashinda TLP, UPDP, DP na wengine mabao ni wa huko huko bara...Ama kweli "fadhila ya punda mashuzi"

    ReplyDelete
  2. we kweli mzanzibari ... fadhira ya punda ni nini !?

    ReplyDelete
  3. Tena Baba na mama, na uzuri zaidi ni kwamba Baba Unguja, Mama Pemba
    Lakini naweza pia nisiwe Mz'bar kwa tafsiri ya baadhi ya watu kama mzee
    Amour Bamba(wa CUF) ambae alidai kwamba mzenj halisi lazima awe na aidha nywele za singa au pua ndefu!

    Ama kuhusu huo msemo, mimi si masikini wa kisw. nna uhuru wa kusema 'fadhila ya punda mashuzi ua mateke' lakn. mashuzi ni maarufu zaidi hasa kwa punda alieshiba na sio "FADHIRA" Mimi si mkurya wala Msukuma kwani hao ndio wenye matamshi ya namna hiyo!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.