Habari za Punde

Hapa na Pale Katika Picha Zenji...

 Mji Mkongwe ni moja ya mitaa yenye vivutio vya utalii katika Kisiwa cha Unguja kwa biashara ya vitu vya kitalii vya aina yote, na mtalii au mgeni anayetembela mitaa ya Mji Mkongwe haondoki bila ya kununua kitu ikiwa ni kumbukumbu yake ya kutembelea Zanzibar na kutoa historia ya maeneo ya historia yalioko katika mitaa hiyo. 
 Mandhari ya majengo ya mitaa ya mjhi mkongwe maeneo ya shangani, hurumzi na Vuga kama inavyoonekana pichani ikiwa na haiba ya kuvutia jinsi ya majengo yake ya gorofa za historia ya mji huo wa kale tangu enzi za mababu majengo yake yanazidi kuvutia wagani wanaotembela mji huo. 
Mdau bado unakikumbuka kibanda hichi cha Urojo cha SEMA TAMU, kwa Ali Kiduchu Kwaboko, kikiendelea na shughuli zake za kuuza urojo kama kazi na kama ulivyokiacha huduma yake iko bomba...

5 comments:

  1. mbona muuzaji siye Ali kiduchu ninaemfahamu mie?

    ReplyDelete
    Replies
    1. uyo ni mteja wa urojo akipata huduma, ali kiduchu bado yupo

      Delete
  2. Naamini miaka 20 ijayo majengo yate ya zamani yatakua yameisha, ii jeuli yenu ipunguwe! Kwa kweli inashangaza huku bara kuna vivutio vya kila aina, fukwe zenye urefu wa km 1400, kilimanjaro, misitu, mito na maziwa na mji wa BAGAMOYO lakini wazungu wengi wanaelekea zazibar, ukiwauliza 'STONE TOWN'.. au wenzetu mnaloga?

    ReplyDelete
  3. Kaka hakuna kuroga, vinjonjo tu hivyo vya kipwani

    ReplyDelete
  4. Yah! Ni thafi na nashkuru sana kuona japo kwa ufupi mandhari ya Zanzibar na jinsi inavyoonekana katika picha hasa kwa oblique, inavutia sana.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.