Na Marzuku Khamis Maelezo Pemba 20/4/2012
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraaza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein amesema kuwa Serikali yake hailitobinafsisha Shirika la Taifa ka Biashara Zanzibar (ZSTC).
Amesema nia na lengo la Serikali ni kuliimarisha Shirika hilo na kuhakikisha kwamba Wakulima wanapata manufaa makubwa ya zao hilo hilo la Karafauu.
Dkt Shein ameeleza hayo leo huko katika Ukumbi wa Kiwanda cha Makonyo Wawi Chake Chake Pemba wakati alipokuwa akiwashukuru Wajumbe wa Kikosi Kazi chaTaifa cha Usimamizi wa zao Karafuu Zanzibar na kuufunga msimu wa uchumaji wa zao hilo japo kuwa ununuzi mdogo wa zao utaendelea.
Amesema kuwa zao la Karafuu unaliingizia Serikali Fedha nyingi ukilinganisha na mazao mengine ya Biashara katika uchumi wa Zanzibar hivyo Serikali itahakikisha kuwa inachukuwa jitahada lzaidi kuona kuwa zao hilo linaimarika kna kuipatia fedha nyingi Serikali.
Amesema kuwa kikosi kazi imefanya kazi ya ziada safari hii katika kulilida zao hilo lisitoroshwe kwa njia ya Magendo hivyo juhudi alisema ziendelezwe katika misimu ujao.
Dkt Shei mbali na hilo ilimu iliotolewa na Kikosi Kazi imesaidia sana katika kuhakiokisha Wakulima wanauza karafuu zao katika vituo vya Shirika la ZSTC.
Mapema Dkt Shein alikabidhiwa na Katibu Mkuu wa Kamati ya Kikosi kazi Julian Raphael Ripoti ya Utekelezaji kazi ya Kamati hiyo juu ya utekelezaji wa kazi yao kwa msimu wa mwaka 2011/2012. Pia na kupewa Zawadi na Meneja wa ZSTC Suleiman Jongo. Vile Vile Naibu Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar Thuwaiba Kisasi kwa niaba ya Wizara hiyo alimkabidhi Mheshimiwa Rais zawadi ya Nembo ya Karafuu.
Wakati huo huo Dkt Shein amesisitiza kwamba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaendelea kuwapatia huduma za lazima Wananchi wa Visiwa vya Zanzibar siku hadi siku.
Dkt Shein aliyasema hayo huko Ziwani alipokuwa akizungumza na Wananchi mara baada ya ufunguzi wa Mradi wa Maji katika Shehia ya Ziwani.
Amesema kwamba lengo la Mapinduzi ya 1964 nikuwapatia Wazanzibari huduma muhimu bila upendeleo na kazi hiyo itaendelea kutekelezwa na Serikali.
Mradi huo umegharimu shs 200Millioni 629 elfu mia sita na kuminanane ambao utanufaisha Wananchi 17elfu wa Shehia tano za Ziwani,Mbuzini,Kianga Ole na Kisiwani.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO PEMBA
20/4/2012
Mheshimiwa Dr Shein kwa wakati huu naunga mkono si sahihi kubinafsisha zao la karafuu hasa kutokana na bei nzuri ambayo serikali yako imewapatia wananchi wako. Natowa tahadhari wale wanaoshadidia kubinafsisha wasome kutokana na Makosa ya Serikali Ya Tanganyika chini ya mkapa wamebinafsisha pamba munaona yanayowafika wakulima kule na pia mashirika asilimia tisiini ya yale yaliyobinafsishwa yamekufa
ReplyDelete