TIMU ya soka ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayoundwa na Watanzania wanaoishi nchini India, imeibuka bingwa wa michuano ya kila mwaka ya inayoitwa ‘The Football 4 Hope-United Cup’ iliyofanyika jijini New Delhi.
Katika mchezo wa fainali uliopigwa katika dimba la Thayagaraj Sports Complex jijini New Delhi, India., Tanzania iliibwaga Botswana kwa mabao 2-1 baada ya mechi kali iliyotoa burudani tosha kwa mashabiki.
Mashindano hayo ya mwaka huu yaliyodhaminiwa na kampuni ya SABMiller, yameshirikisha timu za nchi 14 zenye uwakilishi nchini India.
Tanzania imetwaa ubingwa huo ambao ulikuwa ukishikiliwa na timu ya jumuiya za Umoja wa Mataifa ‘UN Organisations’.
Katika mechi za awali, Tanzania ilizishinda timu za Denmark mabao 11-0, Ufaransa 4-0, India 2-0, Israel 7-1, Hope5-1, Hispania 2-0, China 6-1 na TanzaniaIndia 1-0.
Timu nyengine zilizoshiriki michuano hiyo, zilikuwa Balozi za Misri, Saudi Arabia, Indonesia na Uholanzi.
No comments:
Post a Comment