Habari za Punde

Timu ya Habari Zanzibar Yawasili Visiwa vya Marashi ya Karafuu na Ushindi wa Kishindo.

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar Bihindi Hamad Khamis akipokea Kombe la Ubingwa wa  mpira wa miguu kwa Mwenyekiti wa Timu ya Habari Spots Club ya Zanzibar Issa Ahmada Hija, baada ya kuwasili bandari ya Zanzibar wakitokea mjini Dae-es-Salaam na kupokewa timu hiyo katika Bandari ya Zanzibar ikitokea Dar es salaam, katika mashindano ya Kombe la  NSSF.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Bihindi Hamad Khamis akikabidhiwa  Kombe cha Ubingwa wa mchezo wa Netiboli na Katibu Msaidizi  wa Timu ya Habari Spots Club ya Zanzibar Amina Kapenta baada ya kuwasili katika bandari ya Malindi Zanzibar wakitokea Dar-es- Salaam, katika michano ya NSSF. yaliomalizika hivi karibuni.
Shabiki wa timu ya Habari Hiji Shajak, akifurahia ushindi wa timu yake ya Habari kwa kuibuka na ushindi wa michuano hiyo wakati ilipowasili katika bandari ya Malindui Zanzibar.  
Muangalizi wa Ofisi wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Issa Ismail akiwa na furaha baada ya kuwapokea wachezaji wa Habari spots Club ambao wamerudi kutoka katika mashindano huko Dar es salaam na kufanikiwa kushinda Michezo yote.

Na Faki Mjaka-Maelezo

Timu za Wizara ya Habari,Utamaduni,Utalii na Michezo, Habari Sports na Habari Queen, ambazo zilishinda michuano ya Kombe la NSSF jijini Dar es Salaam zimewasili leo Zanzibar na kupata mapokezi ya aina yake ambayo yaliongozwa na Naibu Waziri wa wizara hiyo Bi Hindi Hamad Khamisi.

Mara baada ya kuwasili bandarini Zanzibar vikosi hivyo vililakiwa kwa ngoma aina ya Boso ambapo wachezaji wa timu hiyo kwa kushirikiana na viongozi wa Wizara hiyo walishiriki kusakata burudani hiyo ya ushindi.


Katika mchezo wa fainali kwa upande wa soka timu ya Habari Spots ilifanikiwa kuwatandika wenyeji wa michuano hiyo timu ya NSSF kwa jumla ya mabao 4-0 katika uwanja wa Sigara-Chang’ombe ambapo kwa upande wa netiboli Habari Queen waliwabanjua kinadada wa TBC kwa magoli 30-10

Akielezea siri ya mafanikio ya ushindi huo Kocha wa Habari Queen Amina Kapenta amesema ushindi wao ulitokana na juhudi na matayarisho ya muda mrefu ambayo waliyafanya kabla na wakati wa mashindano hayo.

Kwa upande wa Soka, Mwenyekiti wa timu hiyo Issa Ahmada amesema nidhamu ya wachezaji na moyo wa kujituma ndiyo iliyokuwa silaha pekee ya kuweza kupata ushindi huo wa kishindo

NSSF ilianzisha mashindano hayo tokea mwaka 2004 ikiwa ni mwaka wa tisa hivi sasa na imepanga kuyaboresha zaidi mashindano hayo kwa kuyafanyia katika mikoa mbali mbali ambapo kuna wanachama wake.

Huu ni mwaka wa pili mfululizo kwa timu ya Habari Queen kunyakua kombe la NSSF ambapo kaka zao Habari Sports ni mara yao ya kwanza kuchukua Kombe hilo tokea kuanza kushiriki.

Imetolewa na Idara ya Habari Maelezo Zanzibar

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.