Habari za Punde

Chenji ya Rada - Zanzibar Tumo?


A K Simai

Kwa wanaofuatilia kwa ukaribu sakata la ununuzi wa rada lililotokea takriban miongo miwili iliyopita tulifurahishwa na uamuzi wa Serikali ya Uingereza kuirudishia “chenji” Serikali ya  Muungano Tanzania baada ya kubainika kuwepo mazingira ya rushwa katika ununuzi wa Rada ile.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliingia mkataba na Serikali ya Uingereza pamoja na BAE Systems kwamba pesa hizi zitakaporudishwa zitumike katika sekta ya Elimu Tanzania.


Majuzi tumepata taarifa ya Mheshimiwa  Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( Tamisemi) Elimu Kassim Majaliwa akitoa ufafanuzi jinsi pesa hizi kiasi cha Bilioni 30 zitakavyotumika.

Alisema Pesa hizi zitanunuliwa madeski katika Mikoa mitatu ya Tanzania Bara nayo ni Mwanza, DaresSalaam na Morogoro. Alisema pesa hizi zitaweza kupunguza tatizo la madeski kwa kiwango cha Asilimia 80.

Pia alisema Shilingi Bilioni 3.2 zimetengwa kwa ajili ya kununu vifaa vya maabara. Na Nyengine ziwekezwe katika kununua vitabu kwa ajili ya skuli za msingi kwa 16000.

Nilikuwa nijaribu kupata maelezo tu vipi katika Chenji ya Rada, Zanzibar tumo au hatumo katika kufaidika na chenji hii.

Kama tumo lini tutaelezwa na Serikali yetu pesa hizi zikikabidhiwa zitatumika vipi? Kwani wenzetu tayari wameweka wazi jinsi chenji hii itakavyotumika. Kwa kuwa sina sehemu ya kuulizia nimeonelea nitumie njia hii ya blog labda wenye uweledi wa mambo wataweza kutujuza au kutusaidia kuweza kupata taarifa

6 comments:

  1. Kero za Muungano, Moja ni Tanganyika kuvaa koti la Serekali ya Muungano. Hakijulikani cha Muungano wala cha Tanganyika. Waziri wa Muungano ndo huyo huyo wa Tanganyika, akenda akiomba msaada, akisafiri hupokewa kama viongozi wa Tanzania na hupewa kama cha Pamoja na Zanzibar hata kama Jambo hilo sio la Muungano.. Wakikipata hukitumia kwa Tangaanyika, Wazanzibari wakiulizia kwa mfadhili huambiwa tushakupeni Tanzania. Kero zilizosimamiwa na vikao zaidi ya 80 na kutumia mamilioni ya Pesa za Walipa kodi Vimeshidwa kutatua Kero hizi miaka 48 sasa.. Walishashauria Serekali Tatu na tume Kadhaa huko nyuma ikiwemo ya Warioba na Kisanga vile vile aliyekuwa Rais wa Zanzibar Jumbe na hili ndio lilimfukuzisha kazi akavuliwa urais Dodoma. Tanganyika Nia yake ni kuimaliza za Zanzibar kwa kujineemesha wao na viongozi ambao wanaolinda Muungano huu kwa Maslaha yao binafsi. Jamhuri ya Watu wa Zanzibar kwanza Watuaachie tupumue..

    ReplyDelete
  2. 'Baniani' mbaya lakini kiatu chake....?
    Kumbe chenji ya rada UWAMSHO mnaitamani... eeh?

    Sasa hivi ndio naanza kupata picha namna W'z'bari tusivyoelewa mambo ya muungano na yale yasiyo ya muungano. Inaonekana bado tunafuata ule msemo wa "chetu, chetu,..chao, chetu"..sababu tu, Bara wanatumia jina la TZA, ambalo ni letu sote!

    Tena 'Bangi' hii mpaka baadhi wabunge wanayo, wakiskia jambo zuri la maendeleo, limeelezwa kwa upande wa Bara japo si la muungano, utaskia wabunge wetu, wanauliza " serikali ina mpango gani kwa upande wa Z'bar?

    Wanajisahau pale pale wanapong'ang'ania kila kitu tuwe na cha kwetu japo uchumi wetu hauruhusu.

    UWAMSHO, wanaruhusu TVZ iendeshwe kienyeji, halafu wafikirie TBC. ni ya muungano!

    UWAMSHO, waridhike Z'bar kua na gazeti moja TV moja na Viredio vya mwisho chumbe halafu wafikirie vile vyombo vya Bara ni vya muungano!

    UWAMSHO, waridhike Z'bar kutokuwa na hosptl. ya rufaa ya uhakika halafu wafikirie MUHIMBIL, na OCEAN ROAD ni za muungano.

    Ni bahati mbaya tu kwamba, jina la serikali ya muungano linatumika pia kwa wizara, idara na taasisi za Bara (zisizokua za muungano)

    Mimi nadhani, wakati umefika kwetu wazanzibari kuwa serious na mambo yetu. Z'bar sasa hivi tuna matatizo mengi kama vile ardhi, matibabu, kilimo, elimu, ajira pamoja na uchumi,wakati huo huo 'population' inazidi kukuwa siku hadi siku.

    Wasomi wanashindwa hata kuitisha kongamano la kitaifa kujadili matatizo mbali mbali yanayotukabili visiwani yakiwemo ya uchumi, utadhani watu hawakusoma, hata ukisikia kongamano hapa ni la kidini au la kisiasa


    UWAMSHO, acheni kuwadanganya watu kwamba haya yote ni matatizo ya muungano' kumbukeni ule msemo usemao "you can fool some pple, some times, but you can't fool all pple, all the times'

    Hizo kero za muungano mnazozisema kila mtu anakiri kwamba zipo lkn. tusitumie hizi kuficha matatizo yetu...au mmetumwa?

    ReplyDelete
  3. Mchangiaji wa pili,tuache tupumue!!
    Sisi (wa-zanzibari wengi), tumeridhika na hao UAMSHO wetu. Kwasababu nyie, wanasiasa 'uchwara/maslahi' ndio mliotufikisha hapa leo hii.

    Na hayo maneno ya bob marley,uliyoya-quote hapo mwisho,basi yanakugusa wewe zaidi, kuliko UAMSHO!

    ReplyDelete
  4. Mimi naamini, wengi kati ya wanachama wa UWAMSHO pia ni wanachama wa vyama vyetu viwili vikubwa hapa Z'bar.

    Sasa kama Waz'bari walio wengi wanaridhika na hoja za UWAMSHO, kwanini basi wasiwatume pia viongozi wao wa kisiasa(wabunge ) wakapeleka hizo hoja zao Bungeni kumaliza 'UDHIA'?

    Maana sasa imekua kama tupo Syria, kila ijumaa dua halafu dua zenyewe reeefu!..kama jana Mselem kanichosha kweli...dua saa nzima ?
    Sasa watoto wetu watakwenda saa ngapi skuli? au ndio mtaka kugeuka TALIBAN na BOKOKHARAM kwamba elimu ya magharibi haifai?

    ReplyDelete
  5. Hongera sana ndugu yangu A. K. Simai kwa mada zako zenye kuleta changamoto, mada za namna hii kama ilivyokua kwa mada yako iliyopita kuhusu kushuka kwa kiwango cha elimu zinangachamsha sana.

    Ni bahati mbaya tu kwamba wengi wetu tunavutiwa na mada za kishabik lakini zile zinazohusu ukweli na ufuatiliaji wa mambo tunashindwa kuzichangia.

    Naamini hata hilo swali lako huwezi kupata majibu ya maana kwa vile wengi wetu hatufatilii mambo.

    Binafsi siku moja nilikua naulizia namna Z'bar tunavyochangia uendeshaji wa wizara za muungano na namna kodi inayokusanywa na TRA-Z'bar inavyogawanywa pamoja na misaada kutoka nje, hakuna aliyejibu.

    Wakati mitandao ya wenzetu kama JAMII FORUM unacho uliza unajibiwa wataalamu wanajitokeza sana kule!..tuseme hapa kwetu ndio hatukusoma au wasomi wetu hawajui kama kuna mitandao ya kijamii au ndio 'ugoigoi tuu!'
    ila ndugu yangu usichoke!

    ReplyDelete
  6. Sasa nadhani SMZ watajua kua makundi ya namna hii si ya kucheza nayo!
    haya dawa yake ni kuya'crush once and for all!

    Haya,.. naskia jioni hii walitaka kuvamia kituo cha polisi! na bado, mwisho wataelekea 'white house!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.