Na Joseph Mwambije, Songea
ASKARI Polisi aitwaye Lucas Komba mwenye namba E9507 Mkazi wa Mkoani Tabora amesambaratishwa kwa risasi baada ya kupigwa risasi na Mkandarasi mmoja, Joseph Mrema (31)kwenye paja la kushoto na kulia wakati askari huyo akimzuia mkandarasi huyo aliyelewa kufyatua risasi ovyo hewani.
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Mrakibu Mwandamizi wa Polisi,George Chiposi tukio hilo lilitokea juzi majira saa 2.45 usiku katika maeneo ya Seedfarm Songea mashariki,Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.
Alisema kuwa Askari aliyesambaratishwa kwa risasi mapajani anafanyia kazi katika Mkoa wa Tabora na hapa Songea alikuja kwa likizo yake kubwa kupumzika na kwamba ndiko alikozaliwa.
Kaimu Kamanda huyo alifafanua kuwa Mkandarasi huyo alitumia silasha aina ya Pisto kufanya unyama huo baada kuwa amelewa pombe na hivyo kufyatua risasi ovyo hewani akitaka kuwazuru watu.
Alisema wakati Mkandarasi huo akifyatua risasi ovyo ndipo askari huyo alimfuata na kumzia na ndipo akamfyatulia risasi zilizomjeruhi.
Alisema kuwa baada ya Askari huyo kujeruhiwa alikimbizwa katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma kwa matibau ambako kutokana na hospitali hiyo kutokuwa na vifaa vya kutosha alipelekwa katika Hospitali ya Misheni Peramiho iliyoko nje ya mji wa Songea.
Kaimu Kamanda huyo alibainisha kuwa Mtuhumiwa huyo atafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili baada ya upelelezi wa Polisi kukamilika.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Hospitali ya Misheni Peramiho, Dkt Venance Mushi amethibisha kupokelewa kwa mgonjwa huyo na kusema kuwa anaendelea vizuri na kwamba ameshafanyiwa upasuaji wa kuondolewa risasi zilizokwama mapajani.
No comments:
Post a Comment