Habari za Punde

Uhaba Walimu wa Sayansi Bado Tatizo

Na Hafsa Golo na Mwajuma Bulaya
TATIZO la uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi unaozikabili skuli za Zanzibar, litadumu kwa muda mrefu endapo serikali haitokuwa na mikakati ya uhakika katika kulimaliza tatizo hilo.

Uchunguzi wa Zanzibar Leo umebaini kuwa endapo serikali haitojifunga kibwebwe kuwa na walimu wa sayansi, Zanzibar itakuwa msindikizaji huku nchi nyengine zikisonga mbele kimaendeleo hasa ikizingatiwa umuhimu wa sayansi katika maendeleo.

Kilio cha walimu wa sayansi kwa skuli za Zanzibar kimekuwa cha muda mrefu ambapo katika uchunguzi wa Zanzibar Leo uliofanywa umebaini sababu kadhaa ikiwemo mishahara na maslahi madogo.

Ofisa wa Elimu ambaye hakupenda kutajwa jina lake, alisema tatizo la uhaba wa walimu linachangiwa na Mamlaka husika kwani walimu hawaoni kama wanathaminiwa.

Ofisa huyo alisema walimu wengi wenye kumudu kufundisha masomo ya sayansi kwa uhakika wameondoka Zanzibar na kukimbilia Tanzania bara kufuata maslahi na mishahara yenye kukithi maisha yao na famailia zao.

“Sikilizeni hili tatizo litaendelea kwa sababu walimu hisia ni kwamba hawathaminiwi, wanalipwa mishahara na kupata maslahi madogo yasiokidhi maisha yao”, alisema Ofisa huyo.

Alifahamisha kuwa udogo wa mishahara umeifanya Zanzibar kuwapoteza walimu wengi na kwenda kufundisha Tanzania bara, huku wakiziacha skuli za Zanzibar zikiwa kwenye hali mbaya ya kukosa walimu hao.

Kwa upande wao walimu wa sayansi, walisema wamekuwa wakikabiliwa na changamoto kadhaa katika ufundishaji wa masomo hayo.

Mwalimu Mpaji Khamis Mohamed kutoka skuli ya Kinyasini Mkoa wa Kaskazini Unguja, alisema tatizo lililopo karibu kwa skuli zote hasa za vijijini ni kutokuwepo kwa vifaa vya maabara.

“Naona kama hakuna tofauti kufundisha sayansi na sanaa, kwa sababu hakuna vifaa vya maabara vya mwanafunzi wa sayansi kufanyia majaribio”, alisema mwalimu huyo.

Aidha mwalimu huyo alisema kutokana na uchache wa walimu wa sayansi, umesababisha walimu wa masomo ya sayansi kufundisha zaidi ya vipindi saba.

“Vipindi vingi vinamfanya mwalimu kushindwa kufundisha kwa umakini, wanafunzi nao wamekuwa wengi, serikali haya lazima iyaone kwa kuyatafutia ufumbuzi”, alisema mwalimu huyo.

Naye Msaidizi Mwalimu mkuu katika skuli hiyo, Haji Majid Haji, alisema tatizo la walimu wa sayansi limekuwa sugu kwani kutokana na uchache wa walimu hulazimika kuwakodi kutoka mjini kufundisha wanafunzi skulini hapo.

Wanafunzi waliozungumza na gazeti hili, walisema sababu ya kuchukia masomo sayansi ni ukosefu wa walimu wazuri wa masomo hayo, hali ambayo huwakimbiza kwenye masomo ya sanaa ili kujinusuru kufeli.

Kwa upande wake Ofisa Elimu sekondari, Khalifa Rashid alisema kutokana na kilio cha muda mrefu juu ya kukosekana kwa walimu wa masomo hayo na vifaa vya maabara, wizara imekuwa kwenye jitihada kubwa za kulipatia ufumbuzi wa tatizo hilo.

Alisema wizara inaendelea na ujenzi skuli za kisasa katika kila wilaya ili kuimarisha masomo hayo na kuwapatia walimu walimu wa kutosha wa masomo hayo katika ngazi tofauti.

Mbali na hayo mwalimu Khalifa alisema ifikapo mwezi Juni skuli hizo zitaanza kufundisha na wizara imefanya juhudi kuwaajiri walimu 10 kutoka Nigeria na wengine 6 kuoka Marekani wenye shahada ya pili katika fani ya sayansi.

Aidha alifahamisha kuwa kuonesha kuwajali waalimu, serikali imeamua kutofautisha mshahara wa walimu wa sayansi na walimu wa masomo ya sanaa, ambapo mishahara ya walimu wa sayansi ipo juu.

Akielezea utaratibu utakaotumika katika kuwapata wanafunzi watakaofanya vizuri kupitia michipuo ya darasa la saba, kidato cha tatu hadi cha tano pia akizitaja skuli ambazo zitawekwa madarasa maalumu ya sayansi kuwa ni Kiembesamaki, Dimani, Kwamtipura, Pajemtule, Uzini, Matemwe, Chaani na Karume.

MASLAHI madogo ya mshahara kwa walimu wa masomo ya sayansi katika skuli za Zanzibar ndicho kikwazo kikubwa kinachosababisha kukosekana kwa walimu hao nchini

Hayo yameelezwa na afisa wa idara ya elimu ya sekondari ambaye hakutaka jina lake kutajwa alisema maslahi madogo ya mishahari yamesabisha kuwakimbiza waalimu wengi wa sayansi hapa Zanzibar na kuelekea Tanzania bara kwa ili wakidhi hali ya maiisha yao.

Afisa huyo alidai kuwa serikali imechukua nafasi kubwa ya kuwapoteza waalim hao kwani walijali zaidi maslahi ya viongozi wa ngazi za juu bila ya kuzingatia mishahara midogo inayowalipa waalim hao ambayo haikidhi mahitaji yao kutokana na ugumu wa maisha.

Walimu mbalimbali wanaofundisha masomo ya hayo walisema kuwa wanapata changamoto nyingi kuanzia maslahiyao na ufundishaji huwa na usumbufu kutokana na uhalisia wa kukokekana kwa vifaa vya mahaba na kupelekea kutokuwa na tofauti ya ufundishaji baina ya masomo ya sayansi na sanaa

Mmoja waalimu hao Mpaji Khamis Mohamed ambaye ni mwalimu wa skuli ya kinyasini Mkoa wa Kaskazini Unguja alisema imekuwa ni tatizo kubwa ambalo hadi leo serikali imekuwa ikisuwasuwa katika kulitafutia ufumbuzi suala hili kwani waalimu wengi wa fani hii hawapo kutokana na ukosefu wa wa kufundisha wanafunzi ili waweze kuwaandaa waalimu wazuri wa baadae.

Alisema imekuwa vigumu kwao katika ufundisha kwani mwalimu mmoja hulazimika kufundisha zaidi ya vipindi saba kwa siku jambo ambalohat huyo mwalimu mwenyewe hushindwa kufundisha vyema kutokana na uhalisia wa uchovu.

Naye Msaidizi wa mwalim mkuu katika skuli hiyo Haji Majid Haji alisema kuwa tatizo hili limekuwa sugu hadi kufikia kukodi walimu wakufundisha masomo kutoka sehemu tofauti ili waweze kuwapatia wanafunzi elimu hiyo ya sayansi.

Na kwa upande wa wanafunzi kutoka katika skuli tofauti walisema kuwa sababu ya kuchukia masomo sayansi ni ukosefu wa waalim wazuri wa masomo hayo na kumepelekea wanafunzi wengi kujiingiza katika masomo ya sanaa.

Naye afisa elimu sekondari Mwalimu Khalifa Rashid alisema kuwa kutokana na kilio cha muda mrefu juu nya kukosekana kwa walimu wa masomo hayo na vifaa vya mahaba wizara ya elimu imenya jitihada za msingi li kupata ufumbuzi wa tatizo hili.

Alisema hivi sasa Wizara imekwishajenga skuli za kisasakatika kila wilaya ili kuimarisha masomo hayo na kuwapatia waalimu walimu wakutosha wa masomo hayo katika ngazi tofauti

Mbali nahayo mwalimu Khalifa alisema ifikapo mwezi juni skuli hizo zitaanza kufundisha na wizara imefanya juhudi kuwaajiri walimu 10 kutoka Nigeria na wengine 6 kuoka Marekani wenye shahada ya pili katika fani ya sayansi.

Pia alifahamisha kuwa ili kuonyesha kuwajali waalimu hawa serikali imeamu kutofautisha mshahara wa waalimu wa sayansi nawaalimu wa masomo ya sanaa hivyo basi kiwango cha walimu wa sayansi kipo juu zaidi ukilinganisha na walimu wa sanaa.

Akielezea utaratibu utakaotumika katika kuwapata wanafunzi watakaofanwa vizuri kupitia michipuo ya darasa la saba, kidato cha tatu hadi cha tano pia akizitaja skuli ambazo zitawekwa madarasa maalumu ya sayansi kuwa ni kiembe samaki,Dimani,Kwamtipura,Pajemtule, Uzini ,Matemwe,Chaani na karume.







2 comments:

  1. Tatizo si uhaba wa walimu, tatizo ni mshahara duni kwa walimu...serikali lazima ijipange vizuri hapa kama wanataka kweli watu wafanye vizuri

    ReplyDelete
  2. Serikali inatakiwa kutofautisha viwango vya mishahara kwa waalimu wa art, science na wale wa masomo ya dini na kiarabu.

    Angalau tofauti baina yao inatakiwa iwe 100,000/ wakati mwingine inavunja moyo, wewe unapiga Math, chem, na physics, mwezako 'hadha waladun' mwisho wa siku tofauti 40,000/

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.