Habari za Punde

Maalim Seif, Akifunguwa Mkutano wa Kongamano la Muungano na Mchakato wa Katiba.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad, akifunguwa mkutano wa Mhadhara wa Wazi wa Mada ya Muungano na Mchakato wa Katiba, uliofanyika katika Ukumbi wa Ecrotanal Zanzibar, ulioandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar kwa kushirikiana Ford Foundation.  
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Profesa Chris Maina Peter, akitowa maelezo kuhusu Mhadhara wa Wazi wa Muungano na Mchakato wa Katiba uliofanyika ukumbi wa jengo la Ecrotanal Maisara.
 Mwakilishi wa Taasisi ya Ford Foundation Kanda ya Mashariki mwa Afrika Maurice Makoloo, akitowa maelezo ya Taasisi yake katika mkutano wa Kongamano la Wazi la Muungano na Mchakato wa Katiba lililofanyika katika ukumbi wa Ecrotanal.
Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar Ibrahim Mzee Ibrahim, akiwasilisha Mada ya Muungano na Mchakato wa Katiba, katika Mhadhara wa wazi ulioandaliwa na Kituo cha Huduma za  Sheria Zanzibar kwa kushirikiana na Taasisi ya Ford Fuondation Kanda ya Mashariki mwa Afrika,katika ukumbi wa jengo la Ecrotanal.   
Mchumi Mselem Khamis Mselem, akichangia Mada ya Muungano na Mchakato wa Katiba baada ya kuwasilishwa na Mkurugenzi wa Mashitaka Zanzibar Ibrahim Mzee.  
Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Harusi Miraj Mpatani, akifafanua mada juu ya Muungano na Mchakato wa Katiba iliowasilishwa na Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar, katika Mhadhara huo uliofanyika ukumbi wa Ecrotanal Zanzibar. 
Washiriki wakimsikiliza Mtoa Mada katika Mhadhara wa Wazi wa Muungano na Mchakato wa Katiba.
Wafanyakazi wa Taasisi ya Ford Fuondation Kanda ya Mashariki mwa Afrika wakimsikiliza Makamu wa Kwanza wa Rais akifungua mkutano huo.
Washiriki wa Mhadhara huu wakifuatilia Mada iliwasilishwa na Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar.
Baadhi ya Viongozi wa Siasa na Dini wakifuatilia michango ikitolewa na washiriki wa mhadhara huo katika ukumbi wa Ecrotanal.
Mdau wa Siasa Mchenga akichangia Mada katika Mhadhara huo.
 Mbambo ya kuchangia mada hayoo..
 Father Peter akichangia mada katika mhadhara wa wazi wa Muungano na Mchakato wa Katiba.
 Mdau wa NGOS Consolata akiwa katika kuchangia mada.

1 comment:

  1. Mmiliki wa blog ni vizuri ukituwekea picha ziwe angalau na kichwa cha habari hizo picha tupu hujuwi zinasema nini au nini kinaendelea. Asante

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.