KIBAHA, Pwani
TIMU ya soka ya Mkoa wa Kaskazini Pemba, imeendelea kuwa ngazi kwa timu pinzani kwenye michuano ya Copa Coca Cola, baada ya jana asubuhi kukubali kichapo cha magoli 3-0 mbele ya Iringa katika mchezo uliofanyika uwanja wa Nyumbu mkoani Pwani.

Timu hiyo iliweza kuwazuia washambuliaji wa Iringa kwa dakika 45 za kwanza tu za mechi hiyo ya kundi B, ambapo timu hizo zilikwenda mapumziko zikiwa hazijafungana.
Katika kipindi cha pili, ilionekaana dhahiri vijana hao kuishiwa pumzi, na hivyo kuruhusu nyavu zao kuchanwa mara tatu, ambapo mchezaji Goodluck Jonas aliipatia Iringa bao la kwanza katika dakika ya 51, Musa Maginga akaongeza mnamo dakika ya 67 kabla Ramadhan Kiwelu kumaliza kazi kwenye dakika ya 70.
Kabla ya ushindi huo, Iringa ilipoteza mechi mbili za kwanza kwa kufungwa mabao 3-0 na Mjini Magharibi, na baadae kusaluimu amri mbele ya Mwanza kwa kipigo cha 3-1.
Nayo Kusini Pemba katika mechi ya kundi A iliyochezwa uwanja wa Tanganyika Packers ulioko Kawe, Dar es Salaam, iliambulia sare ya kutokufungana na Ilala, ambapo mjini Kibaha kwenye uwanja wa Tamco, Dodoma iliinyoa Mtwara kwa bao 1-0.
Katika uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, Tabora iliichapa Shinyanga mabao 2-0.
No comments:
Post a Comment