Habari za Punde

TRA: Mapato yanayokusanywa Zanzibar yanatumika Zanzibar

Na Hafsa Golo
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imesema inatekeleza majukumu yake Zanzibar, huku maofisa wake wakilazimika kuvumilia kejeli na maneno ya kashfa kutoka kwa baadhi ya wateja.

Ofisa wa Elimu kwa walipa kodi wa Mamlaka hiyo ofisi ya Zanzibar, Saleh Haji alielza hayo jana mjini hapa alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi huko Gulioni.

Alisema baadhi ya watu wakiwemo wafanyabiashara wamekuwa wakiiona TRA kama adui wa uchumi wa Zanzibar, kwa kuhamisha fedha kupelekwa bara.

Alifahamisha kuwa ipo kasumba iliyojengeka miongoni mwa jamii ambayo sio ya kweli kuwa TRA Zanzibar makusanyo ya fedha inayoyafanya Zanzibar inayapeleka Tanzania bara.

“Wananchi wanauelewa mdogo dhidi ya TRA kwa kuonekana kuwa makusanyo ya fedha wanayoyafanya Zanzibar yanakwenda serikali ya Muungano, jambo ambalo halina ukweli”,alisema ofisa huyo.

Aidha alifahamisha kuwa ufahamu huo mbaya umekuwa ukiwasababishia kukumbana na maneno mbali mbali ya kashifa, kejeli na kuonekana kama wasaliti wanapotekeleza wajibu wao.

Ofisa huyo aliwatoa hofu wananchi wa Zanzibar kuwa TRA haisafirishi
hata senti tano kwenda Tanzania bara, ambapo makusanyo ya Zanzibar yamefunguliwa akaunti maalum katika benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ).

Saleh alifahamisha kuwa msimamizi wa fedha zinazokusanywa na TRA Zanzibar ni katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha Uchumi na Mipango ya Maendeleo kutoka serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

“Baada ya kukamilika kwa utaratibu wa fedha tunazozikusanya kila mwisho wa mwezi huishia katika mfuko wa hazina wa Zanzibar, huu ndio ukweli hakuna fedha zinazokwenda Tanzania bara”,alisema ofisa huyo.

Alisema kasumba mbaya zinazofanywa dhidi ya TRA zimekuwa zikisababisha kushuka kwa mapato kwani baadhi ya wafanyabiashara wanakwepa wakidhani fedha hizo huishia Tanzania bara.

Ofisa huyo alisema kuwa jitihada kubwa zinahitajika kuchukuliwa katika kuielimisha jamii ya Zanzibar ili iweze kuelewa kwa undani utekelezaji wa majukumu ya TRA visiwani hapa na kuondokana na mitazamo na fikra potofu.

“Nawasihi wananchi tubadilishe fikra kwa kuwa na mtazamo chanya dhidi ya Mamlaka na mapato inayoyakusanya, kejeli na maneno mabovu hayatatufikisha katika harakati za kimaendeleo ambazo zinahitajiwa na wananchi wote”,alisema.

Aliishauri serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuliweka bayana suali la mapato ya TRA Zanzibar kwa kuwafahamisha wananchi matumizi ya fedha hizo.



12 comments:

  1. Kwani ni lazima TRA ikusanye mapato Zanzibar? Kwa nini isiwe ZRB tu ndio chombo pekee chenye mamlaka ya ukusanyaji mapato Zanzibar?

    ReplyDelete
  2. Nafikiri it does not matter nani anakusanya as long as zinaishia kwenye hazina ya SMZ. Nafikiri cha muhimu kama alivyosema huyo mtu wa TRA Zanzibar, serikali itoe kauli iseme kuwa ni kweli kuwa pesa zote zinazokusanywa na TRA Zanzibar zinatiwa katika mfuko wa serikali ya SUK. Mimi ninavyojua ni kuwa watu wakilipia TRA wanalipa through BOT Zanzibar.

    ReplyDelete
  3. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  4. Uwelewa wangu ni kwamba, TRA inakusanya mapato ya kodi ZILIZOKUBALIWA na KATIBA ya Tanzania, kwamba ni za MUUNGANO, ambazo ni KODI ZA FORODHA (Customs/Trade Taxes) na KODI YA KIPATO (Income Taxes). Kodi nyingine zote pamoja na VAT, Stamp Duty na Usajili wa namba za magari kwa upande wa Zanzibar, zinakusanywa na ZRB.

    Kuhusu kwa nini isiwe ZRB tu ndio chombo pekee chenye kukusanya mapato hapa Zanzibar, nadhani ni jambo linalowezekana. Lakini, tunapaswa pia kujiuliza ni kwa nini MAJIMBO yetu ya uchaguzi yana MBUNGE na MWAKILISHI? Watu wawili kwa jimbo moja, ni sawa?

    ReplyDelete
  5. Wewe ndugu yangu, mchangiaji wa kwanza(UWAMSHO) kama kweli Z'bar inakuuma na sisi inatuuma hivyo hivyo, hatutaki ZRB iwe ndio chombo pekee cha kukusanya mapato, tumechoka kuona watu wakifanya ufisadi uliokithiri bila hata kukemewa.

    Watu wanapora utafikiri serikali haipo, kazi yao kujenga majumba na kununua mashamba, Kisakasaka yote wameinunua wao. Kwetu sisi, uharibifu ni uharibifu tu bila kujali nani anaeufanya.

    Mchangiaji wa pili umeeleza vizuri lkn. kuna kitu kidogo hakipo sawa;
    Watu wanaolipa kodi za TRA Z'bar wanalipia kwenye ofisi zao zilizopo MAYUGWANI karibu na Msikiti mabluu.

    TRA ndiwo wenye A/C B.O.T Z'bar kama ilivyo seria za mawizara na mashirika ya umma

    ReplyDelete
  6. Mambo haya yalianza pale Komandoo, aliposhindwa kuwalipa wafanyakazi wa Z'bar mishahara yao kwa miezi mitatu na kwenda kutaka msaada Bara ndio akaulizwa namna anavyousanya kodi na tukasaidiwa na TRA

    ReplyDelete
  7. Hii nayo ni kero nyengine ya MUUNGANO huu.
    Dawa ni kuuvunja tu, na kero zote za Muungano zitakuwa marehemu.

    ReplyDelete
  8. We, CALYPSO, usikimbilie matusi, tizama na hicho kizungucho kwannza.."Is really matter, ha.. nkizungu cha wapi hicho? au cha utaani?

    Mara ya pili utasema 'it really matters'..na kesho!!!..UWAMSHO wee!

    ReplyDelete
  9. doesnt matter as long as ujumbe umefika maswala ya lugha doesnt make any sense.

    ReplyDelete
  10. Mishikioyoooo!.., sema na hilo ntatizo lamuungano!

    ReplyDelete
  11. Adhubany ama adhabugani wewe TRA inakuhusu nini kama Mzanzibari na unafaidika nayo vipi? Wenzako wako katika Bunge la Afrika Mashariki huko sasa wewe umo na una tele yasiohusu huo Muungano wa ukusanyaji mapato!?

    ReplyDelete
  12. Ndugu yangu UWAMSHO, kwangu mimi TRA ni kama ilivyo kwako, ni mamlaka ya kukusanya mapato, ambayo mwisho wa siku yanakabidhiwa kwa SMZ kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli mbali mbali za kiserikali.

    Kuhusu bunge la Afrika Mashariki ni kweli mimi simo lkn. naamini wamo W'bari ambao wanatuwakilisha mimi na wewe na pia kama kuna mambo yasiyohusu muungano ndani ya A.mashariki ni suala la viongozi wetu tuliowachagua kusema ukweli.

    Mimi, ndio maana mara nyingi nikiona mambo yanaharibika, hukimbilia kulaumu utendaji wa SMZ, wabunge na wawakilishi wetu badala ya kuwauliza watu kama wanutaka au hawautaki.

    Kuna matatizo 'lukuki' hapa nyumbani ambayo yamo ndani ya uwezo wa SMZ lkn. kwa makusudi nyinyi UWAMSHO mnatumia uwezo wetu mdogo wa elimu kutwambia ni matatizo ya muungano. lkn kwa kutumia 'common sense' tunaona ni matatizo ya SMZ.

    UWAMSHO, mimi naijua Z'BAR na SMZ na Viongozi wake kuliko wewe na kama huwajui vizuri basi subiri ukaribie uchaguzi wa 2015!

    Mimi, wasiwasi wangu ni kwamba kama mkihubiri chuki, kufukuza watu na kuchoma makanisa tutakuja kukimbilia wapi?..wakati nyinyi mnasifia mshikamano visiwani wengine bado wananyimwa vitambulisho vya Mzanzibari ukaazi.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.