Habari za Punde

China kuisaidia Zanzibar kukabiliana na maafa


Na Othman Khamis, OMPR
BALOZI Mdogo wa China aliyepo Zanzibar, Chen Qiman amesema serikali ya Jamhuri ya watu wa China itaendelea kuinga mkono Zanzibar katika harakati za kimaendeleo, kiuchumi na namna ya kukabiliana na maafa.

Balozi huyo alieleza hayo jana wakati alipokutana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, kumpa mkono wa pole kufuatia janga la kuzama kwa meli ya MV. Skagit lililotokezea wiki iliyopita.

Balozi Chen alisema China itapanua wigo katika masharikiano yake na Zanzibar na kwamba itaangalia uwezekano wa kusaidia namna ya kukabiliana na majanga pale yanapotokezea.

Balozi huyo alisema tukio la kuzama kwa meli ya MV Skagit limeihuzunisha sana wanachi wa China na kwamba hali ya huzuni waliyonayo Wazanzibari ndiyo waliyonayowa wananchi wa China.

“Wananchi wa Jamuhuri ya Watu wa China wanajua hali ya huzuni iliyoikumba jamii ya Watanzania hasa Wazanzibari kutokana na msiba huo wa kuzama kwa meli iliyosababiha vifo vya wananchi kadhaa”,alisema Balozi huyo.

Katika ziara hiyo Balozi Chen, aliambatana na Uongozi wa Kampuni za Ujenzi za China zinazofanya kazi hapa Zanzibar za Railway Jiangchang Engineering Co Ltd na ile ya Beijing Construction Engineering Group ambazo zote zimekabidhi mchango wa shilingi milioni 5 kila moja.

Kwa upande wake, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, aliipongeza serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China kupitia Balozi zake nchini Tanzania kwa jitihada zake za kuunga mkono harakati za maendeleo.

Balozi Seif alisema kutokana na tukio hilo, serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, imeanza kuchukua hatua mbali mbali za kujihami na kuepuka maafa wakati yanapotokezea majanga.

Alisema serikali kupitia ushirikiano wa pamoja wa Mamlaka za Usafiri wa Baharini za bara (Sumatra) na ile ya Zanzibar (ZMA) zitawajibika kuvifanyia uchunguzi vyombo vyote vya usafiri wa baharini.

“Wamiliki wa vyomo vya usafiri wa baharini lazima wafuate sheria na taratibu za Mamlaka ya usafiri wa Baharini kwa lengo la kuepuka maafa yanayoweza kukingika”, alisema Balozi Seif.

Wakati huo huo, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikutana na Mkurugenzi anayeshughulikia masuala ya Afrika na Carribean wa Umoja wa Ulaya (EU), Fransisca Mosca hapo ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.

Katika mazungumzo yao Balozi Seif aliuomba Umoja huo wa Ulaya kuangalia uwezekano wa kusaidia Zanzibar kutafuta mbinu za upatikanji wa usafiri wa uhakika kati ya Unguja na Pemba.

Alisema serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inakusudia kununua me

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.