Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed
Shein amemteuwa Juma Khamis Juma kuwa Mwenyeikiti wa Bodi ya
Uhaulishaji Ardhi,Zanzibar.
Kwa mujibu wa Taarifa iliotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na
Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Dkt Abdulhamid Yahya Mzee ameeleza
kuwa uteuzi huo ni kwa mujibu wa uwezo aliopewa Rais chini ya Sheria
Namba 8 ya mwaka 1994 kama ilivyorekebishwa Sheria namba 10 ya mwaka
2007 ya uhaulishaji wa Ardhi-Zanzibar.
Uteuzi huo unaanza leo tarehe 30Julai, 2012
Baada ya juhudi kubwa za wawakilishi hatimae Mwenyekiti wa bodi ya uhaulishaji ndio ameteuliwa.
ReplyDeleteKwa kipindi cha takriban miezi sita, Z'bar imekaa bila ya chombo halali cha kusimamia'transfer of properties' halafu eti watu wanadai kua matatizo yetu yanatokana na muungano.
Right, first we have to deal with our own issues and then to look ahead
ReplyDelete