Na Mwashamba Juma
WAZIRI Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Fatma Abdulhabib wa Ferej, amesema inakataza matumizi, njia na zana za uvuvi ambazo zinaharibu mazingira.
Waziri huyo alieleza hayo jana katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi alipokuwa akijibu suali la Mwakilishi wa nafasi za Wanawake Asha Abdu Haji ambaye alitaka kujua kama zipo njia mbadala kwa ajili ya wavuvi.
Waziri huyo alisema serikali haijapiga marufu uvuvi wenye kuzingatia uhifadhi na zana zinazokubalika, ila kinachokatazwa ni matumizi ya njia na zana zisizokubalika.
Alifahamisha kuwa serikali itaendelea kupiga vita kwa nguvu zote matumizi ya zana zisizokubalika kwenye shughuli za uvuvi.
“Nawaomba na kuwasihi sana wananchi wenye tabia ya kutumia njia za uvuvi zinazoharibu mazingira na badala yake watumuie zinazokubalika”, alisema waziri huyo.
Alisema Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais itaendelea kushirikiana na wizara ya Mifugo na Uvuvi katika kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kuachana na uharibifu wa mazingira na faida ya kuyalinda na kuyatunza mazingira ya bahari.
Alisema kupiga marufuku matumizi ya zana na njia za uvuvi zisizokubalika yamelenga kulinda uharibifu wa matumbawe.
Wizara Kuvifanyia Matengenezo Vituo vya Afya
NAIBU waziri wa Afya Dk. Sira Ubwa Mamboya amesema wizara imekuwa ikivifanyia matengenezo vituo vya afya ili kuipunguzia mzigo hospitali ya Mnazi Mmoja.
Naibu huyo alieleza hayo jana katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi alipokuwa akijibu suali la Mwakilishi wa nafazi za Wanawake, Mwanaidi Kassim Mussa.
Katika suali lake Mwakilishi huyo alitaka kujua mipango iliyowekwa na wizara hiyo katika kuviimarisha vituo vya Afya.
Alisema katika kuipinguzia mzigo hospitali ya Mnazi Mmoja, wizara imepanga kuviimarisha vituo vya afya vilivypo mjini kama vile Mpendae, Kwamtipura, Jang’ombe, Amani na Chumbuni.
Aidha alisema wizara hiyo pia itaviimarisha vituo vya wilaya Magharibi vikiwemo Chukwani na Mbuzini.
Alisema katika mwaka 2011/2012, hospitali ya Mnazi Mmoja imehudumia wagonjwa 97,206.
Wananchi Wwanaoishi Nyumba za Mazizini Kuhamishwa
WANANCHI wanaokaa kwenye nyumba za viongozi waliopo Mazizini watahamisha ili nyumba hizo zifanyiwe matengenezo hali itakayowezesha viongozi wa serikali kupatiwa makaazi.
Naibu waziri wa Ardhi, Makaazi Maji na Nishati, Haji Makame Mwadini alieleza hayo jana katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi, alipokuwa akijibu suali la Mwakilishi wa nafasi za Wanawake Panya Ali Abdalla.
Katika suali lake Mwakilishi huyo alitaka kujua mipango ya wizara hiyo katika kuwapatia makaazi vingozi wa serikali.
Alisema baadhi ya nyumba hizo za serikali wanazoishi wananchi ziko katika hali nzuri na zile zilizokatika hali mbaya zitavunjwa na kujenga tena
Alifahamisha kuwa serikali inatafuta eneo jengine la kujenga nyumba za makaazi ya viongozi wa serikali.
Naibu huyo alisema serikali inatumia fedha nyingi kuwakodia viongozi kwa ajili ya makaazi yao na suali hilo litapatiwa ufumbuzi kwa kuwepo kwa utaratibu wa kuwajengeza nyumba viongozi hao.
Akijibu suali la nyongeza lililoulizwa na Omar Ali Sheh, aliyetaka kujua ni kiasi serikali inatumia katika kuwalipia nyumba viongozi.
Waziri wa wizara hiyo, Ramadhan Abdalla Shaaban alisema malipo ya nyumba kwa viongozi wa serikali hayafanywi na wizara hiyo bali kila kiongozi hufanyiwa malipo na wizara yake.
No comments:
Post a Comment