Na Mwandishi Wetu
HATIMAYE timu ya soka ya Jamhuri imepumua baada ya kupata mkopo wa dola elfu nne ili ilipe faini iliyopigwa na Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF).
Itakumbukuwa kuwa, Jamhuri ilipigwa faini na CAF baada ya kuoneshwa kadi nne za njano katika mchezo mmoja mwanzoni mwa mwezi wa Machi, ilipopambana na Hwangwe FC katika Kombe la Shirikisho.
Katibu wa Jamhuri Ahmed Omar, ameliambia gazeti hili jana kuwa, Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), kimeikopesha timu yake dola 2,500, na msamaria aliyekataa kutajwa jina ametoa mkopo wa dola 1,500, huku viongozi na wanachama wa timu wakichangishana dola 1,000.
Omar amesema tayari wamezituma fedha hizo makao makuu ya CAF jijini Cairo, kupitia benki ya Barclays.
Aliishukuru ZFA chini ya Rais wake Amani Makungu, pamoja na wadau wengine walioisaidia timu yake kuondokana na deni hilo kwa CAF ambalo ilipewa hadi Julai 30, kulipa, vyenginevyo lingepanda mara mbili.
KARMA YA UONGOZI: SOMO KWA WANAOHAMASISHA MAANDAMANO
-
Na Mwandishi Wetu
NAJIULIZA maswali ya msingi, kama raia mwenye tafakuri na uzoefu katika
uongozi: je, wanaohamasisha maandamano ni wapinzani, wanaharakat...
6 hours ago

No comments:
Post a Comment