Habari za Punde

Wananchi watakiwa kujitokeza kwa wingi kuhesabiwa sensa ya watu na makaazi


Na Abdi Suleiman, Pemba                              

Wananchi mbali mbali kisiwani pemba, wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuhesabiwa, katika zoezi zima la sensa ya watu na makaazi linalotarajiwa kuanza Augosti 26 mwaka huu nchini Tanzania.

Wito huo umetolewa na mwenyekiti wa kamati ya kuhamasisha sensa wilaya ya chake chake, ambaye pia ni mkuu wa wilaya hiyo, Mwanajuma Majid Abdalla, kwanyakati tofaouti wakiti alipokuwa akiwahamasisha wananchi juu ya kujitokeza kwa kushiriki kuhesabiwa katika zoezi la sensa.

Mwenyekiti huyo alisema kuwa, sensa ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi kwani huiwezesha serekali kupanga mipango yake mbali mbali ya kuwaletea wananchi maendeleo, hivyo ni wajibu kwa kila mwananchi kushiriki katika zeozi hilo.


Alifahamisha kuwa, bila ya sensa maendeleo ya nchi hayatopatikana, kwani idadi ya watu ndio inayopelekea serekali kuweza kuwapatia wananchi wake maendeleo, “huku akitolea mfano kujengwa wa skuli, hospitali, maji safi na salama, barabara, nk yote hayo yanatokana na idadi ya watu baada ya kupatikana kwa takuwimu za sehemu zao”alisema mwenyekiti mkuu wa wilaya ya chake chake.

Alieleza kuwa, kuna baadhi ya wananchi wameitia sensa katika mambo ya siasa, kituambacho sio hivyo, kwani sensa ni kitu muhimu katika serekali kwa ajili ya kupanga mipango yake ya maendeleo na wananchi kuweza kunufaika na mandeleo hayo.

“lengo la sensa ni kuhakikisha wananchi wanahesabiwa, ninalolihimiza wananchi wetu waone sensa inaumuhimu kwa maendeleo ya nchi, na sisi wenyewe kuanzia kwenye shehia, wadi wilaya na mikoa”alisema mkuu wa wilaya.

Alisema kuwa bila ya mashirikiano na wananchi basi sensa haiwezi kufanikiwa, kwni “sasa hivi kumeingi vikundi vya watu chochote kinacholetwa na serekali huviingiza katika mambo ya siasa hasa hii ni kitu ambacho hakiwezekani:alifahamisha.

Aliwataka wananchi kuchukua mfano hali ya baraza la wawakilishi lilivyo muda huu, ambapo wajumbe wameweka siasa zao pembeni na kuwakitu kimoja katika suala la kuwaletea maendeleo.

Umefika muda sasa kwa wananchi kuanchana na siasa katika sula la kuleta mamendeleo ndani ya nchi, ‘baraza lina wajumbe wa vyama tofauti pale wanacho simamia ni maendelo ya nchi au majimbo yao sio siasa kwani sia ipo na kila mtu anayomoyoni mwake”alisema mkuu wa wilaya.

Hata hivyo aliwataka wananchi kuiga mfano wa viongozi wao katika baraza la wawakilishi juu wa kuhimiza maendeleo katika nchi, kwani mashirikiano ya pamoja ni muhimu katika kufanikisha zoezi zima la sensa ya watu na makaazi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.