Na Bakari Mussa, Pemba
Wanaushirika wa Upandaji Mwani wa kikundi
cha Jitihada katika Shehia ya Kiungoni Pemba, wameiomba Serikali kupitia Wizara
ya Mifugo na Uvuvi , kuwapatia taaluma
na Nyenzo za Ufugaji wa Majongoo na Kaa ili waweze kuongeza kipato chao.
Wakizungumza na mwandishi wa Habari hizi
huko Kijijini kwao Kiungoni , walisema kuliko tija wanayoipata kutokana na
kuongezeka kwa gharama za Vifaa na bei ndogo wanayouza kwa wanunuzi.
Wanaushirika hao walieleza kuwa ni
wameamuwa kujiajiri kupitia Kikundi chao kwa kutekeleza Miradi mbali mbali kama vile Uvuvi ambao walipata msaada wa Vifaa kupitia
MACEMP, lakini kwa sasa Vifaa hivyo havitoshi kutokana na mahitaji ya
Wanakikundi.
Hata hivyo walieleza kuwa wanachohitaji kwa
sasa ni kupatiwa Boti yenye uwezo wa kufika mbali ili waweze kupata Samaki wa
kutosha kwa vile waliyonayo haina uwezo wa kufika masafa ya mbali wakati masafa
ya karibu kila mmoja anavua.
Wanaushirika hao walisema kuwa iwapo
watapatiwa miradi mbadala , wanaweza kupiga
hatuwa kubwa katika kupiga vita Umaskini wa kipato.
Walieleza kuwa ni vyema bei ya Mwani iliopo
sasa ikaongezwa kutoka Tsh,400/= hadi 1000/= kwa kilo ,kwani kazi ni kubwa na
Vifaa wananunuwa wenyewe.
Hivyo walisema kuwa wamekuwa na mafanikio kiasi fulani kwani
wameweza kutumia fedha wanazozipata katika miradi yao kuwaendeleza kimaisha na kuepukana na
utegemezi hasa kwa akinamama.
No comments:
Post a Comment