Habari za Punde

Mfuko wa Vyombo vya Habari vya Tanzania Wawapiga Msasa Waandishi Zanzibar u

 Mkurugenzi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) Ernest Sungura, akitowa maelezo ya mfuko huo jinsi ya kuomba Fedha kwa ajiuli ya kufanya uchunguzi wa habari na kuzitowa kwa jamii,wakati wa mafunzo jinsi ya kuandaa mpango wa kuomba fedha hizo kwa waandishi wa habari wa Zanzibar. 


 Mkufunzi wa habari za uchunguzi kupitia Redio Edda Sanga, akitowa mafunzo hayo kwa waandishi wa habari wakati wakifanya mahojiano wanapokuwa katika maeneo ewanayotembelea kuandika majina kwa uhakika na kurejea kuhakiki habari zao kabla ya kuziwasilisha.
 Mkufunzi wa Mafunzo ya kutayarisha maombi ya kuandika habari za Uchunguzi Ndimara Tegambwage, akisisitiza jambo wakati wakitoa muelekeo wa utayarishaji wa maombi ili kupata fedha katika mfuko wa vyombo vya habari Tanzania (Tanzania Media Fund) wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari wa Zanzibar katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Mazizini Zanzibar.


 Mwalim Rashid Omar akichangia katika mkutano huouliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Beach Mazizini.
 Mhariri Mtendaji wa Shirika la Magazeti ya Serekali Zanzibar Zanzibar Leo Abdallah Mohammed, akichangia katika mkutano huo kuhusu ufadhili kwa Vyombo vya Serekali, katika mfuko huo.
Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali Zanzibar wakiwa katika Mkutano wa kuboresha habari za Uchunguzi, ulioandaliwa na Tanzania Media Fund, katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Beach Mazizini ili kuwawezesha waandishi kuandia habari za uchunguzi zilizo bora kwa jamii.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.