Habari za Punde

Mkutano wa kamati Kuu ya CCM Waendelea



 Wajumbe wa Kamati Kuu Taifa,(CCM) wakiwa katika ukumbi wa Mkutano kabla ya kuanza kwa kikao hicho leo,kilichoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete. [Picha na Ramadhan Othman,Dodoma.]

 Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete,(katika) akifungua kikao cha siku moja,katika ukumbi wa White House Mjini Dodoma leo,(kushoto)Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Dk. Ali Mohamed Shein,[Picha na Ramadhan Othman,Dodoma
 Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete,(katika) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Dk. Ali Mohamed Shein,( kushoto)Katibu Mkuu wa CCM Taifa Willson Mkama,(kulia) wakifurahia jambo wakati Mwenyekiti allipokuwa akiendesha Kikao cha siku moja cha Kamati Kuu kilichofanyika leo katika ukumbi wa White House, Dodoma. [Picha na Ramadhan Othman,Dodoma.]

Na Rajab Mkasaba, Dodoma
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeendelea na vikao vyake chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete hapa mjini Dodoma na kueleza kufurahishwa kwake kwa kujitokeza wanachama wengi ambao wamegombea nafasi za uongozi ndani ya chama hicho wakiwemo wasomi.
Hayo aliyasema Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete, wakati akifungua kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (CC),
Kikao hicho kimeendelea baada ya kumalizika kikao cha Kamati ya Maadili ya CCM, kilichofanyika kwa muda wa siku tatu mfululizo ambacho kilimalizika majira ya saa tisa za usiku wa kuamkia leo
Katika maelezo yake, Mwenyekiti huyo wa CCM Taifa, alieleza kuwa kutokana na wagombea kuwa ni wengi ndio sababu kubwa iliyopelekea kikao hicho cha Kamati ya Maadili ya CCM, kichukue muda huo mkubwa huku ikizingatiwa kuwa inapitia jina la kila mgombea wa nafasi za uongozi ndani ya chama hicho ambayo ameigombea.
Alisema kuwa wanachama wanaokaribia 5000, wamegombania nafasi mbali mbali za uogozi ndani ya chama hicho zikiwemo nafasi za Jumuiya za CCM.
Aidha, alisisitia kuwa chama hicho kinaendelea kusonga mbele huku akiwashangaa wale wanaosema kuwa chama hicho kinakufa.
Alisema kuwa katika kikao hicho cha Kamati ya Maadili ya CCM, kilichomalizika kimefanya kazi kubwa ikiwa ni pamoja na kuja na mapendekezo kadhaa.
Wakati huo huo,Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisisitiza kuwa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (CC) na Halmashauri Kuu (NEC) vitahakikisha vinatenda haki kwa wagombea wote.
Nape alisema kuwa Kamati ya Maadili ya CCM ilitakiwa kufanya kikao kimoja kwa ajili ya kupitia na kutoa mapendekezo ya wagombea lakini kutokana na wingi wao kamati hiyo imelazimika kuchukuwa siku tatu kufanya kazi hiyo muhimu ndani ya chama hicho.
Pamoja na hayo, Nape alieleza kuwa chama hicho kimepokea uamuzi wa Kinana kwa heshima kubwa kwa kutambua muda mrefuambao alikitumikia chama kwa uadilifu mkubwa
Pamoja na hayo, Mwanasiasa Mkongwe nchini, Abdulrahman Kinana alieleza kutogombea tena nafasi ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) na kusisitiza kuwa licha ya kungatuka kwake ataendelea kutoa mchango wake kwa Chama pamoja na Taifa kwa jumla.
Alieleza kuwa hatowania tena nafasi hiyo kwa sababu miaka 25 aliyoshikilia nafasi hiyo inatosha na kusisitiza kuwa kitendo chake hicho kinatoa nafasi kwa wanaCCM wengine hasa vijana kutoa michango yao ndani ya chama hicho kwani wapo wengi wenye sifa na uwezo wa kuongoza chama.
Wajumbe mbali mbali wa Kamati Kuu (CC), wanaendelea na kikao hicho mjini hapa akiwemo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.