Na Haji Nassor, Pemba
JUMLA ya nyumba 364 kati ya 546 hazina hazina vyoo na
wakaazi wake wanaendelea kujisaidia msituni na kando kando ya bahari, huko
Shehia ya Kiwani, Wilaya ya Mkoani Kisiwani Pemba.
Akiuzugumza na
mwandishi wa habari hizi kijijini huko Sheha wa shehia hiyo, Abdallah Makame
alisema kua kati ya nyumba hizo zenye vyoo ni nyumba 182, huku hali ya
kukabiliwa na maradhi ya mripuko ikiwanyemelea wananchi wake.
Alisema kutokana
na idadi kubwa ya nyumba kukosa vyoo, wengi wao hulazimika kufanya haja kubwa
pembezoni mwa mkaazi yao na wengine hufanya
shughuli zao katika maeneo yao ya kazi kama vile kando kando ya bahari.
Sheha Abdallah
alieleza kua juhudi kubwa zimekuwa zikichukuliwa wa na hata Serikalia za mitaa
ili kuwahamasisha wananchi kuchimba vyoo na kunaongezeko la vyoo takribani 70
katika mwaka uliomalizika.
Alisema kutokana
na wataalamu wa afya kupita mara kwa mara na kuhamasisha matumizi bora ya vyoo,
kwa sasa wananchi hususani wanaojenga nyumba mpya hulazimika kutenga sehemu ya
choo.
‘’Bado, kwa mujibu
wa idadai ya nyumba zilizomo ndani ya shehia yangu kama
ni 182 tu zenye vyoo hali hairidhishi , illa kasi ya kuchimba kwa sasa
imeongezeka mara dufu’’,alifafanua sheha huyo.
Akizungumza
uharibifu wa mazingira shehiani humo alieleza kuwa bado elimu haijawafikia vya
kutosha wananchi wake na wamekuwa wakidhani suala la ukataji miti haliingia
miongoni mwa kadhi ya kusababisha joto.
Alieleza ingawa
elimu imekua ikitolea lakini si kwa kiwango kikubwa na bado wapo baadhi ya
wananchi wamekuwa wakikata miti kwa kasi kwa madai ya kukosa jambo jengine la
kufanya.
‘’Wapo wanaofanya
biashara ya miti na wapiga mkaa , hawa bado masikio yao ni mazito maana hujibu kwamba ndimo
wanapojiatia riziki sasa wanapoaachia kazi hiyo hulala na njaa’’,alizidi kusema
Sheha huyo wa Kiwani.
Hata hivyo
ameziomba taasisi za Serikali na watu binafsi kwenda kijiji huko ili kuwazindua
wakaazi wa shehia yake ili kuondokana na ukataji miti na kuhamasishwa kupanda
mipya kwa kasi.
Aidha amewataka
wananchi kuacha tabia ya kuchoma moto ovyo hasa katika kipindi hiki cha
kiangazi kwani majanga kama hayo katika
kipindi hiki hujitokeza mara kwa mara.
No comments:
Post a Comment