BAADA
ya kukaa takriban wiki mbili wananchi wa Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini
Pemba, kukosa huduma ua umeme kufuatia transfoma iliokuwa ikisambaaza umeme
kuungua, hali hiyo sasa imetuwama kufuatia Shirika la Umeme Zanzibra kufunga
transfoma mpya.
Hafla ya ufungaji wa mashine hiyo mpya, ilifanyika
jana mbele ya uongozi wa Wilaya na wananchi kadhaa waliohudhuria kutokana na
kukosa huduma hiyo tokea katikati ya mwezi huu jambo lilizorotesha shuguli
zinazotegea nishati hiyo ikiwa ni pamoja na Hospitali.
Akizungumza na waandishi wa habari mara
baada ya kukamilika kwa kazi ya ufugaji wa transfoma hiyo na huduma hiyo
kurejea katika halia yake ya kawaida, Msaidizi Afisa Uhusiano wa ZECO tawi la Pemba , Faki Othuman Sharif alisema kuwa jumla ya shilingi
20 milion zilitumika kununua mashina hiyo.
Alisema kuwa fedha zote hizo zimetolewa na
ZECO ambapo mashine hiyo mpya (100 kv) ilinunuliwa Mkoani Arusha Tanzania bara na inauwezo mkubwa wa kusambaaza
huduma ya umeme katika eneo hilo
la Micheweni.
Faki alieleza kuwa, Shirika la Umeme kwa
sasa limejipanga vyema katika kutoa huduma bora kwa wananchi na ndio maana muda
mfupi tu, tokea kuungua kwa transfoma hiyo ikaharakisha kurejesha huduma kwa wananchi.
‘’Sisi Shirika la umeme kwa sasa
tumejipanga vyema, maana dharura kama hizi wala hatuwashirikishi wananchi kama lazima watoe fedha, illa ZECO ndio hugharamia fedha
zote na kuhakikisha tunawarejeshea wananchi huduma’’,alifafanua .
Aidha aliwataka wananchi wa maeneo mbali
mbali kuhakikisha wanatoa taarifa za haraka Shirika la Umeme pale ambapo
kumejitokeza hitalafu ya umeme badala ya kukimbilia kwenye vyombo vya habari
ambapo msaada wake huchelewesha.
Hata hivyo ameupongeza uongozi wa Wilaya ya
Micheweni na wananchi wote, kwa kuwa wastahamilivu katika kipindi chote cha
ukosefu wa huduma hiyo, hadi hapo juzi iliporejea kama
kawaida.
‘’Katika hili tunampongeza sana Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Juma
Abdallah (mzee wa busara) kwa kuwatuliza wananchi wakati sisi ZECO, tulipokuwa
katika mchakato wa kutafuta transfoma mpya’’,alizidi kufafanua.
Wakizungumza na mwandishiwa habari hizi,
baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Micheweni walielezea kufurahishwa kwao na ZECO
kwa kutimiza ahadi yao kama
walivyoahidi juu ya kurejesha huduma hiyo.
Walisema kuwa kwa sasa Serikali kupitia
Shrika hilo la
Umeme, limejipanga kwa nia thabiti ya kuwaletea maendeleo wananchi na kutimiza
ahadi wanazozitoa ambapo ni tofauti na miaka mengine.
Mutribu Hamad Mabarouk alisema kuwa, hawakutarajia
kuwa huduma hiyo ingeweza kurudi juzi, kwani walidhani kuwa ahadi iliotolewa ni
ya kuwatuliza wananchi na ingechukua hata wiki tatu.
Nae Mwanafunzi wa Skuli ya Micheweni
sekondari anaesoma darasa la kumi na moja (FIII) Issa Omar Fundi, alisema kuwa
kwa sasa wamepata matumaini maana hata kwa wale waliokuwa wakiendelea na masomo
ya usiku majumbani yatarudi kama kawaida.
Shirika la umeme Zanzibar ZECO, limekuwa
halina utaratibu wa kuwachangisha fedha wananchi pale transfoma inapoungua au kuharibika,
ambapo mchango hujitokeza iwapo wananchi wameomba transfoma kwa ajili ya
kuunganisha huduma ya umeme katika vijiji vyao.
sijui mpaka lini watu wataacha kufanyishwa kazi kienyeji, hakuna cha gloves, miwani wala kofia ngumu......tutafika?
ReplyDelete