Habari za Punde

‘Polisi Jamii Cup’ mwendo mdundo

 
Na Kauthar Abdalla
 
TIMU ya soka ya Taifa Zanzibar iliyo chini ya miaka 17, imeanza vyema michuano ya kuwania kombe la polisi jamii, baada ya kuilaza kombaini ya Polisi bao 1-0 kwenye uwanja wa Ziwani.
Bao hilo pekee liliwekwa nyavuni na mchezaji Ali Omar katika dakika ya 28 baada ya kuipenya ngome ya Polisi.
Michuano hiyo inashirikisha timu za shehia 84 za mkoa wa Mjini Magharibi, yakihusisha vijana waliomo kwenye vikosi vya ulinzi shirikishi.
Mashindano hayo yalifunguliwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Yussuf Omar Chunda, alilipongeza jeshi la Polisi kwa kubuni mpango wa ulinzi shirikishi, ambao alisema umesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza vitendo vya uhalifu kwenye shehia mbalimbali Unguja na Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.