Marehemu. Joseph Moses Castico
Historia fupi ya marehemu Joseph. Moses. January Castico.
Marehemu Joseph Castico ni mtoto wa Sita katika Familia ya Mama Christina Mary Ali, na mtoto wa Kwanza wa Mzee Moses Joseph Castico.
Amezaliwa tarehe 27-4-1952, katika hospitali ya Mnazi Mmoja, na kupata Elimu yake ya Msingi katika Skuli ya Convet Tumekuja na kuendelea na elimu yake ya msingi katika skuli ya St.PaulKiungani Unguja
Amepata elimu ya Sekondari katika skuli ya Lumumba kidatu cha Nne hadi cha sita.
Elimu ya Juu amepata katika Chuo cha Ualimu Bet-el-Ras Zanzibar na kuendelea na mafunzo ya Ualimu katika Chuo cha Ualimu Dar-es-Salaam na kupata shahada ya kwanza ya Ualimu.1975/1976
Marehemu Joseph Castico amepata mafunzo nje ya Nchi katika Nchi za Urusi,Sweden,Norway,India, Uarabun na kutembelea Mikoa ya Tanzania Bara kwa shughuli za Kikazi na Mafunzo.Alikuwa Mfanyakazi bora wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, na kufikia ngazi ya Ukurugenzi katika Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo. amepata tunzo mbalimbali wakati wa uhai wake na kuwa mfanyakazi bora mara mbili .
Alikuwa mwanamichezo na Mwanamuziki na Mtungaji wa mashairi wakati wa uhai wake. Akiwa katika harakati za kuchapisha kitabu chake kinachosubiriwa kwa hamu na wasomi mbalimbali hapa Zanzibar kikiwa katika harakati za kuanza kuchapishwa kinachoitwa RAMCO.
Hadi mauti yanamkuta amekuwa na Cheo cha Msaidizi Mtendaji Kituo cha Kiswahili Ecrotanal Zanzibar, na Mwenyekiti wa ZIFF, Mjumbe wa BUSARA Zanzibar.
Marehemu amebarikiwa kupata Watoto watano na Wajukuu Wanne.ameacha Mke .
Marehemu ameuguwa kwa mudu mfupi baada ya kuuguwa hafla shindikizo la Damu hadi kumkuta mauti tarehe 21-9-2012 katika Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja Zanzibar juzi saa moja Usiku.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA MAPENZI YA BWANA YATIMIZWE.
REST IN PEACE CASTICO.
ReplyDeleteUlitufundisha Michezo ya umiseta ili tuweze kucompete na maskuli mbali mbali Tanzania bara na visiwani.