Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Balozi wa Rwanda Nchini Tanzania DKt.Ben Rugangazi,Ikulu Mjini Zanzibar jana.[Picha na
Ramadhan Othman,Ikulu.]
Ramadhan Othman,Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akifuatana na Balozi wa Rwanda Nchini Tanzania Dkt.Ben Rugangazi,Ikulu Mjini Zanzibar jana,baada ya mazungumzo yao.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
RWANDA imevutiwa na mafanikio yaliofikiwa na Zanzibar katika sekta ya utalii na kueleza kuwa iko tayari kupanua wigo katika sekta hiyo ikiwa ni pamoja na kukuza ushirikiano kwenye sekta nyengine ambazo zitaimarisha utalii.
Hayo yalisemwa leo na Balozi wa Rwanda nchini Tanzania Dk. Ben Rugangazi wakati alipokuwa na mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Ikulu mjini Zanzibar, alipofika kwa ajili ya kujitambulisha.
Katika mazungumzo hayo, Dk. Rugangazi alimueleza Dk. Shein kuwa Rwanda imo katika mchakato mkubwa wa kuimarisha sekta ya utalii nchini humo lakini bado ina mengi ya kujifunza kutokana Zanzibar kupata kupata mafanikio makubwa.
Alisema kuwa Zanzibar imepata mafanikio makubwa katika sekta hiyo ya utalii ambayo imekuwa ikichangia kwa kiasi kikubwa pato la taifa na kusisitiza kuwa mikakati ya nchi hiyo ya hivi sasa ni kukuza sekta nyenginezo zikiwemo mawasiliano na usafiri ambazo zinzweza kuleta mchango mkubwa katika uimarishaji wa sekta hiyo.
Aidha, Dk. Rugangazi alieleza kuwa nchi yake imo katika hatua za kuimarisha mawasialino ya usafiri wa anga hali ambayo itaimarisha zaidi sekta hiyo ya utalii nchini humo na hata kutoa ushirikiano na nchi jirani zilizopata mafanikio kama Zanzibar.
Alieleza kuwa mbali ya sekta hiyo ya utalii nchi yake imekusudia kuimarisha uhusiano na ushirikiano katika sekta ya elimu ikiwa ni pamoja na mashirikiano ya elimu juu.
Balozi Rugangazi alisema kuwa suala la utamaduni nalo lina umuhimu katika kuimarisha mashirikiano na kukuza uhusiano kati ya nchi mbili hizo na kusifu hatua zilizochukuliwa na Zanzibar katika kukuza, kuuenzi na kuuendeleza utamaduni wake wa asili.
Balozi huyo wa Rwanda nchini Tanzania, alitoa pongezi kwa uongozi wa Jamhuri ya Tanzania tokea wakati wa Rais wa Mwanzo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayari Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambae aliimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano na nchi hiyo.
Alieleza kuwa Rwanda hivi sasa iko salama na inaimarisha amani na utulivu uliopo na kusisitiza kuwa matukio ya uvunjifu wa amani nchini humo yatabaki kuwa historia.
Alisema kuwa Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kuiunga mkono Rwanda katika kuimarisha sekta zake za maendeleo zikiwemo sekta ya biashara, usafiri na usafirishaji hasa ikizingatiwa kuwa nchi hiyo inatumia zaidi bandari ya Dar-es-Salaam kwa kusafirishia bidhaa zake kadhaa.
Sambamba na hayo, Balozi huyo alisema kuwa mchakato wa kuanzishwa kwa reli na usafiri wa barabara kati ya nchi yake na Tanzania pamoja na nchi nyengine zilizomo ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kutasaidia kupanua sekta ya biashara pamoja na kukuza uhushaino na ushirikiano kati ya wananchi wa nchi hizo.
Kwa upande wake Dk. Shein alimkaribisha Balozi huyo Zanzibar na kumueleza kuwa Zanzibar inathamini uhusiano na ushirikiano mkubwa kati yake na Rwanda.
Dk. Shein alimueleza Balozi huyo kuwa Tanzania ni swahiba mzuri wa Rwanda hatua ambayo imeweza kukuza uhuano na ushirikiano kwa muda mrefu huku akitoa pongezi kwa nchi hiyo chini ya uongozi wa Rais Paul Kagame kwa maendeleo yaliofikiwa ikiwa ni pamoja na uhifadhi wa mazingira na usafi wa mji wake Mkuu wa Kigali.
Dk. Shein alimueleza Balozi huyo kuwa mafanikio yaliofikiwa na Rwanda katika suala zima la uhifadhi wa mazingira na usafi wa mji wake imeweza kuipelekea Zanzibar nayo kupanua wigo kwa kuwapeleka baadhi ya Maafisa wake kwenda nchini humo kujifunza hatua zilizofikiwa na nchi hiyo hata kufikia hapo walipo hivi sasa.
Akieleza kuhusu haja ya kuimarisha mashirikiano katika sekta ya utalii Dk. Shein alisema kuwa hatua za makusudi zimechukuliwa katika kuimarisha sekta hiyo hapa nchini hivyo kuwepo kwa mashirikiano hasa katika sekta ambazo zinaimarisha utalii kutasaidia kwa kiasi kikubwa.
Dk. Shein alisema kuwa kuwepo kwa usafiri wa anga wa moja kwa moja kati ya Zanzibar na Rwanda nako kutakuwa chachu katika uimarishahi wa sekta hiyo ya utalii kwa pande mbili hizo pamoja na kuimarisha na kukuza ushirikiano wa kibiashara.
Kwa upande wa sekta ya elimu Dk. Shein alieleza kuwa ipo haja ya kuimarisha mashirikiano kati ya Rwanda na Zanzibar hasa katika kubadilishana uzoefu wa wakufunzi sambamba na wanafunzi wenyewe kupata fursa ya kubadilishana uzoefu.
Kwa upande wa utamaduni Dk. Shein alimueleza Balozi huyo kuwa Zanzibar ina mengi katika utamaduni wake ambapo juhudi za makusudi zinaendelea kuchukuliwa katika kuuimarisha, kuukuza na kuuendeleza.
Pamoja na hayo, Dk. Shein alimueleza Balozi huyo kuwa Zanzibar nayo inaendeleza amani na utulivu uliopo hapa nchini na mafanikio makubwa yameweza kupatikana katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar yenye Muundo wa Umoja wa Kitaifa kwani wananchi wamekuwa na matarajio makubwa juu ya serikali yao hiyo.
Aidha Dk. Shein alitumia fursa hiyo kutoa shukurani kwa Ras Kagame kwa kuendelea kuyadhamini mashindano ya ‘Kagame Cup’, ambayo yameweza kuwakutanisha vijana wa nchi za Afrika Mashariki na kuweza kuzidisha uhusiano na ushirikiano mkubwa
No comments:
Post a Comment