Habari za Punde

Mamia Wahudhuria Mazishi ya Mke wa Waziri Nyanga na Mtoto wa Rais Mstaafu wa Zanzibar Mzee Jumbe. Migombani

 Viongozi wa Serekali Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Rais Mstaaf wa Tanzania Alhaj Mzee Ali Hassan Mwinyi na Rais Mstaaf wa Zanzibar Mzee Aboud Jumbe akiwa amekaa katika kiti na Wananchi mbalimbali wakijumuika katika maziko ya marehemu, Mke wa Waziri wa Kilimo na Misitu Suleiman Othman Nyanga,  Hanifa Aboud Jumbe, yaliofanyika  nyumbani kwao migombani mjini Zanzibar leo.

 Shekh, akisoma dua baada ya mazishi ya Mke wa Waziri wa Kilimo na Misitu Suleiman Othman Nyanga, Hanifa Aboud Jumbe, yaliofanyika katika viwanja vya migombani. 
Wananchi wakihudhuria maziko ya Mtoto wa Rais Mstaaf wa Zanzibar Aboud Jumbe Mwinyi, Hanifa Aboud Jumbe, Mke wa Waziri wa Kilimo na Misitu Zanzibar Suleiman Othman Nyanga, yaliofanyika nyumbani kwao migombani mjini Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.